WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdillahi Jihad Hassan amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Uteuzi huo aliufanya kwa mujibu wa hati ya sheria namba 111 ya mwaka 2011 ambayo inaruhusu kuundwa kwa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, ilisema walioteuliwa ni pamoja na Ahmed Hussein Chwaya kwa nafasi ya mtaalamu na mshauri wa mambo ya dijital na Ahmed Makame Haji.
Aidha wengine walioteuliwa na waziri huyo ni pamoja na Hamida Ahmed Muhammed kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar kilichopo Tunguu na Said Hassan Said kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Aidha taarifa zilisema kwamba uteuzi huo umefanyika kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Tatu Ali Abdalla alieteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, hivi karibuni

wajumbe wa bodi ya shirika kama ZBC, chombo ambacho ndio kwanza kimeanza na kinatarajia kujiimarisha na hatimae kujitegemea. nilitarajia kusikia majina mzito ikiwezekana kutoka ndani na nje ya visiwani.
ReplyDeleteHuenda wangetusaidia kukifanya chombo hiki kutokua, mwisho 'chumbe' na hatimae kuwafanya watumishi wake waweze kupata kazi ktk mashirika ya nje ya Z'bar.