Msimamo wa matokeo ya Ligi Kuu ya Zanzibar katika mzunguko wa pili
Mchezaji wa timu ya Mundu Kani Alex, akijaribu kuwapita mabeki wa timu ya Mafunzo katika mchezo wa ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Mao, timu ya Mafunzo imeshinda 5--0
Mchezaji wa timu Mundu Patrick James (kushoto) na wa timu ya Mafunzo mwenye jezi ya kijani Said Mussa, wakigombe mpira katika mchezo wa ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Mao, timu ya Mafunzo imetoka kifua mbele kwa kushinda 5--0.
Beki wa timu ya Mafunzo Ali Juma, akiondoa mpira golini kwake kuipusha lawama, huku mchezaji wa timu ya Mundu Ame Juma, akijaribu kumzuiya katika mchezo wa ligi Kuu ya Zanzibar timu ya Mafunzo imeshinda 5 -- 0.
Mchezaji wa timu ya Mundu Patrick James, akijiandaa kuzuia mpira katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar na huku mchezaji wa timu ya Mafunzo akijiandaa kumzuiya, timu ya Mafunzo imeshinda 5 -- 0
Viongozi wa timu ya Mundu hawamini macho yao kuona timu yao imeshindwa kutamba mbele ya maafande wa Mafunzo kwa kuchapwa mabao 5--0, katika mchezo wa ligi kuu ya zanzibar.
Mchezaji wa timu ya Mundu Ame Juma akimpita beki wa timu ya Mafunzo Mohammed Abdulrahaman, katika mchezo wa ligi kuu ya zanzibar uliofanyika uwanja wa mao.
Mchezaji wa timu ya Mafunzo Jaku Juma akimtoka beki wa timu ya Mundu Diku Juma.
No comments:
Post a Comment