Habari za Punde

Matukio Hapa na Pale Mitaani Zenj.

Mfanyabiashara ya Kofia anayetembeza mikononi ilibidi kusita kufanya biashara yake ili kujua matukio yanayotokea Duniani na Nchini kwa kusoma vichwa cha habari za magazeti mbalimbali, katika moja ya kituo cha kuuzia magazeti Kisiwandui.
Leo Biashara Ngumu, ndivyo inaelekea Mfanya biashara huyu wa matunda ya Mapeyasi katika soko la Mwanakwerekwe akitafakari biashara yake, kama alivyokutwa na mpiga picha hii sokoni hapo.  
Wafanyabiashara ya matunda mbalimbali katika soko la mwanakwerekwe wanaopanga nje ya soko hilo inabidi wachukuwe tahadhari ya biashara yao ikatika kipindi hichi cha mvua za masika zinazotarajiwa kuaza hivi karibuni, kuweza kupanga bidhaa hizo juu badala ya chini ili kuepusha mripuko wa matumbo wakati huo.
Mdau unakumbuka zile enzi zetu wakati wa msimu wa zambarau unapoanza? huwa na ajali nyingi za kuanguka katika mizambarau kwa kufuatia vitori nchani mwa matawi.Watoto hawa wakiwa na vipakacha vya zambarau wakitafuta wateja kipakacha kimoja huuza shilingi 1000/=  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.