Habari za Punde

Waziri Jihad Azindua Bodi ya Utangazaji ya ZBC


Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdillah Jihad Hassan akitoa hotuba katika uzinduzi wa Bodi ya Z.B.C huko katika Ukumbi wa ZBC Radio Rahaleo Zanzibar.Kulia kwake ni katibu Wizara hio Ali Mwinyikai na Kushoto yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZBC Tatu Ali, 
~
Waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Bodi ya Z.B.C Wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na michezo Abdillah Jihad Hassan hayupo Pichani akitoa hotuba na kuizindua rasmi Bodi hio.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI ALI MAELEZO ZANZIBAR.

Na Faki Mjaka-Maelezo

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Abdillahi Jihad Hassan amewataka Wajumbe wa Bodi ya Utangazaji ya Shirika la Habari Zanzibar (ZBC)kuwa makini katika kuendesha Shirika hilo ili liweze kuleta maslahi kwa Taifa.

Jihad ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua Bodi hiyo inayoundwa na Wajumbe saba katika ukumbi wa ZBC Radio Raha leo Mjini Zanzibar.

Amesema Jamii ya wazanzibari imejawa na matumaini makubwa na Bodi hiyo ambayo ndiyo mdomo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivyo ubinafsi katika Chombo hicho ni jambo ambalo linapaswa kuepukwa


Amesema jukumu kubwa la Bodi hiyo ya Utangazaji Zanzibar ni kuchochea maendeleo na kuielimisha jamii ambayo imejawa na hamu kubwa ya kutaka kujionea utendaji kazi wa Bodi hiyo

Aidha amefahamisha kuwa ili malengo waliyojiwekea yaweze kupatikana Wajumbe wa Bodi hiyo wanapaswa kufanya kazi kwa mashirikiano na kuwajibika ipasavyo katika majukumu waliyopangiwa kwa mujibu wa taratibu.

Ameongeza kuwa patakapokuwa na mashirikiano na uwajibikaji ni wazi jamii itabadilika jambo ambalo litapelekea pia Bodi hiyo kuweza kuheshimiwa na kufanya kazi kwa urahisi

Nao wajumbe wa Bodi hiyo wamemuahidi Waziri huyo kuzifanyia kazi nasaha zake alizozitoa na kuahidi ufanisi katika kazi zao ili kuliletea Taifa maendeleo.

Bodi ya Utangazaji ya Shirika la Habari Zanzibar (ZBC) inaundwa na Wajumbe saba ambao ni Hassan Mitawi,Ahmed Makame,Yussuf Chunda,Hamida Ahmed Mohammed,Hassan Mzee,Ahmed Chwaya ambapo Mwenyekiti wake ni Tatu Ali.

Imetolewa na Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.