WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, jana amekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi 26 milioni kwa wananchi wa Jimbo la Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba, kwa ajili ya ununuzi wa mashine za kusukumia maji maji.
Profesa Mnyaa alikabidhi hundi hizo kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Chokocho (JUMACHO) huko Michenzani Mkoani, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo hilo hata kama hakuchauguliwa kuwa mbunge.
Akikabidhi hundi tatu ikiwa moja ina thamani ya shilingi 10 milioni na hundi mbili zikiwa na thamani ya shilingi nane milion ,Profesa Mnyaa alisema mashine hizo zitakazonunuliwa ni kwaajili ya visima viwili vya kiji cha Michenzani na Chokocho.
Alifahamisha kuwa kisima cha Chokocho kitasambaza maji katika kijiji cha Chokocho na Kisiwapanza wakati kisima cha Michenzani kitasambaza maji maeneo ya Michenzani pamoja na Kisiwa cha Makoongwe mara mashine hizo zitakapofungwa.
Mnyaa alieleza kuwa utakapomalizika ujenzi wa visima hivyo kutaondosha kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salamakatika Jimbo la Mkanyageni.
“Tutahakikisha kila kijiji tumefikisha maji na tumeweka mifereji, hatutaki kuwaona akina mama wanateseka na wanahangaika kwa kutafuta huduma ya maji”, alisisitiza Profesa Mnyaa.
Katika hatua nyengine Waziri huyo wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia aliwakemea baadhi ya wanasiasa wanaoongoza wananchi kwa kuwapiga propaganda tu bila ya kuwaletea maendeleo endelevu wananchi.
Alifahamisha kuwa kiongozi mzuri ni yule anaeongoza kwa mfano, kuonesha njia na kuwaletea maendeleo wananchi wake, “viongozi wenu mlionao hawafai, wamepewa milioni 25 za Jimbo zikowapi?, alihoji Mnyaa.
Mapema Profesa Mnyaa alikagua ujenzi wa kituo cha afya Michenzani ambao anaufadhili yeye mwenyewe, ambapo jumla ya shilingi milioni 22 tayari zimeshatumika kwa ajili ya kituo hicho na unatarajiwa kutumia milioni 110 hadi kumalizika kwake.
Nao wananchi wa Jimbo la Mkanyageni wamemshukuru Profesa Mnyaa kwa juhudi zake za kuwaletea maendelea wananchi wa jimbo hilo katika nyanja mbali mbali ikiwemo elimu, afya na maji.
Tulitarajia Mh. Habib Mnyaaa(Mbunge wa Cuf) ndio ayafanye hayo lkn. wapi,yanafanywa na yule ambae alinyimwa kura!
ReplyDelete