Habari za Punde

Wake wa Viongozi wazipiga Tafu Soba House Zanzibar.

MKE wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Asha Balozi Seif  Iddi kulia,akimkabidhi Vyarahani,nyuzi za kushonea,Mchele.Sabuni  pamoja na Sukari,kiongozi wa vijana walioacha kutumia madawa ya kulevya na kujifunza tabia njema Fatuma Sukwa,hafla hiyo ilifanyika Detroit Sobar House Mpendae jana,(Picha na Abdallah Masangu
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akiwa na Wake wa Wabunge na Wawakilishi  wakitembelea maonesho ya Vitu  mbalimbali  vya  Sanaa ya Mikono  vinavyotengenezwa na Vijana wa Soba House wakiwa katika vituo hivyo vya  kupata mafunzo ya kuacha matumizi ya Dawa za Kulevya.  

Rais wa Nyumba za Soba House Zanzibar Suleiman Maulid, akipokea moja ya vifaa kutoka kwa Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, alipofika kutembelea vituo hivyo na kujionea kazi za vijana hao wakiwa katika nyumba hizo  jinsi wanavyopata mafunzo ya kazi za Amali kuwasaidia wanapomaliza muda wao wa  ushauri wa kuacha matumizi ya dawa za kulevya. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake kwa Vijana wanaoishi katika Vituo vya Soba House, alipofika kuwazawadia zawdi mbalimbali za Vifaa vya kazi za mikono na Chakula., villivyotolewa na Wake wa Viongozi.
Rais wa Soba House Suleiman Maulid, akitowa historia ya nyumba za Soba House na mafanikio yao walioyapata kwa vijana wanaoamu kuacha matumizi ya Dawa za Kulevya , akiwa yeye ni mmoja ya vijana vijana waliofanikiwa kuacha kutumia dawa za kulevya na kuanzisha vituo hivyo kwa kuwasaidia vijana wezake kuachana na matumizi hayo.
Wake wa Wawakilishi na Wabunge wakiwa katika hafla hiyo ya kutowa msaada kwa vijana wa Soba House.
Vijana wa Soba House wakimsikiliza Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Ali Iddi akitowa nasaha zake kwa vijana hao wanaoishi katika nyumba za Soba House. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.