Habari za Punde

Dk Shein Aendelea na Ziara Kisiwani Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Mkoa huo,katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba jana,(kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Hamadi Mberwa Hamadi, na (kushoto) Mkuu wa Mkoa huo Dadi Faki Dadi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akiangalia Sabuni iliyotengenezwa katika kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa,ambayo inayozalisha sabuni kwa kutumia mashine maalum,alipokuwa katika ziara ya kutembelea maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba,(kulia) Mkurugenzi Mkuu George M.Buchwafwe.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa kuanzisha bednki ya Jamii ya Muwape Saccos Mtemani Wete Pemba, alipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Kijamii Mkoani humo,(kulia) Mize Khamis.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mtoto Suleiman Shaaban Juma, pamoja na wanachama wa Kampuni ya Mkipi Miliki Tungamaa, kuzindua Mradi wa uzalishaji wa sabuni kwa kutumia mashine maalum ya Mkipi Miliki,jana akiwa katika ziara kisiwani Pemba, kuangalia maendeleo ya jamii.

1 comment:

  1. Nakupongeza rais Shein, hivyo ndivyo kiongozi anavotakiwa awe, yaani kuwa karibu na wananchi kwani kukaa ikulu tuu inakuwa vigumu kuelewa matatizo ya watu huko chini ni vizuri ujinee mwenyewe kwani watendaji wa hapo katikati wanakuwa hawakuambii ukweli wanakueleza yale ambayo unapenda kuyasikia, kwa kweli wewe ni kiongozi wengine huwa ni watawala

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.