Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wananchi Uchumi na Ushiriuka.Mhe Haroun Ali Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na Kutunukiwa Nishani ya Southern and Eastern Africa Consortium for Monitering Education Quality.Taasisi inayoangalia na Kupima Ubora wa Elimu kwa Nchi 15 za Kusini na Mashariki ya Afrika. mazungumzo hayo yamefanyika katika Wizara hiyo Mwanakwerekwe Zanzibar. 
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wananchi Uchumi na Ushiriuka.Mhe Haroun Ali Suleiman, akiwaonesha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Nishani ya Southern and Eastern Africa Consortium for Monitering Education Quality.Taasisi inayoangalia na Kupima Ubora wa Elimu kwa Nchi 15 za Kusini na Mashariki ya Afrika. mazungumzo hayo yamefanyika katika Wizara hiyo Mwanakwerekwe Zanzibar.
Wandishi wa Habari wakichukuwa habari katika mkutano na Waziri haroun kutowa shukrani kwa Wadau wa Elimu walioshirikiana nao kufanikisha kupata Nishani hiyo.
Watendaji wa Wizara hiyo wakimsikiliza Mhe Waziri akitowa shukrani wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa wizara hiyo mwanakwerekwe.
Maratibu wa taasisi hiyo Sebtuu Mohammed Nassor akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Taasisi hiyo ilifanya tafiti tatu kwa nchi wanachama wake ikiwemo ya kwanza iliyoangalia uwezo wa kusoma na kuandika kwa wanafunzi wa skule za msingi.
SACMEQ yamtunuku nishani waziri Haroun
Na Mwashamba Juma
WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman, ameishukuru taasisi inayoangalia na kupima ubora wa elimu kwa nchi 15 za Kusini na Mashariki mwa Afrika SACMEQ kwa kuelewa na kutambua mchango wake.
Aliyasema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari ukumbi wa mikutano ofisini kwakwe, Mwanakwerekwe wilaya ya Magharibi.
Waziri Haroun alisema kutunukiwa kwa medani hiyo ni dhahiri kwamba taasisi ya SACMEQ ilitambua mchango wake mkubwa alioutowa na kuona utendaji wake katika taasisi hiyo muda wote wa uongozi wake, wakati alipokuwa waziri wa Elimu miaka 10 iliyopita.
Alisema medali hiyo ni muhimu na ni ukumbusho katika historia ya maisha yake, pia imeijengea sifa nzuri nchi ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi imekuwa nchi wanachama kwa taasisi hiyo.
Medali hiyo iliyotumwa na mkurugenzi wa taasisi ya SACMEQ Damas Makua ambae alimkabidhi waziri wa elimu wa Tanzania Bara, Shukuru Kawambwa kwa kumkabidhi Waziri Haroun.
Nae aliyekuwa maratibu wa taasisi hiyo Sebtuu Mohammed Nassor alisema taasisi hiyo ilifanya tafiti tatu kwa nchi wanachama wake ikiwemo ya kwanza iliyoangalia uwezo wa kusoma na kuandika kwa wanafunzi wa skule za msingi.
Akifahamisha tafiti ya pili Sebtuu alisema taasisi hiyo ilijikita katika somo la hesabati kwa madarasa ya sita pamoja na utafiti uliohusisha masomo ya sayansi kwa skuli za msingi.
Sebtuu alisema kwa Zanzibar tafiti hizo ziligundua tatizo la ukosefu wa vitabu lilizorotesha sekta ya elimu kwa kipindi hicho na baadae ilipochapisha vitabu vingi vya madarasa ya sita na saba.
Aidha kutokupata mafunzo kwa walimu wa skuli za msingi lilikuwa ni tatizao lililogunduliwa kutokana na tafiti hizo, hiyo taasisi ilitowa mafunzo kwa walimu ili kutatuta tatizo kwa walimu wa nchi wanachama wa taasisi hiyo.
SACMEQ ni taasisi iliyojikita katika utafiti wa elimu na kuona ubora wa elimu katika nchi za Kusini na Mashariki ya Afrika ikiwa na makao makuu yake nchini Uingereza, ambapo waziri Haroun alikuwa waziri anaewakilisha mataifa ya nchi za Mashariki mwa Afrika.
Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1993, ambapo ilianza na nchi wanachama 6 wakiwemo Kenya, Zanzibar, Zambia, Zimbabwe, Malawi, na Mauritius, na baadae kuengezeka nchi wanachama wakiwemo Namibia, Seychelles, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania bara, Uganda, Msumbiji, Botswana na Lesotho.
Ndio maana taasisi nyingi za kiafrika haziheshimiki duniani kutokana na mabo kama haya!
ReplyDeleteMtu, kama Haruna anastahili nishani kweli? Huyu aliwahi kua waziri wa elimu kipindi cha 'ujahil' na kutumia siasa kuvuruga mfumo wa elimu: kwa mfano wakati wa 'ajira za kama' alijaza watoto wa form 2 MKRUMAH ili wasomee uwalimu, na pia aliwaacha wanafunzi kusoma DINI na KIARABU,ili apate akijisifu kwa kupasisha wanafunzi wengi FORM 5 NA 6.
Matokeo yake sasa Watoto wameshamaliza Degrees za DINI na KIARABU Chukwani SMZ inakataa kuwaajiri.eti wabaki kulinda maadili ya jamii...walinde na njaa?