HOTUBA
YA MHESHIMIWA NAIBU WAZIRI WA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO MH. THUWAYBAH KISSASI
KATIKA UZINDUZI WA IJITIMAI YA KIMATAIFA FUONI - UNGUJA TAREHE 29-APRIL-2012.
Bismillahi Rahmani Rahim
Amir
Mkuu wa Fiiysabililah Tabligh Markaz Zanzibar,
Ndugu Viongozi mbali
mbali,
Maamiri, Masheikh , Maduati, Tull-bul ilmu na
Wageni waalikwa wote,
Ndugu Waumini mabibi
na mabwana mliofika katika ulingano huu kutoka kwa Mola wetu
Assalamu Aleykum
Warahmatullahi Wabarakatuh”
Ndugu zangu katika Uislam
Kwanza
kabisa nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu alieturuzuku neema
kubwa ya uislamu; na akatuwezesha kukutana katika uzinduzi wa ijitimai yetu hii
pahala hapa pa kheri tukiwa wazima na wenye Amani.
Pia
Rehma na Amani zimshukie Kiongozi wetu na Kigezo chetu, Mtume Muhammad (S.A.W),
jamaa zake, Masahaba zake, wafuasi wake, pia wazee na Masheikh wetu wote walio
hai na waliokwisha kutangulia mbele ya haki.
Ndugu zangu katika Uislam
Kwa
kuitikia amri ya Mtume (S.A.W) isemayo “Hamshukuru
Mwenyezi Mungu asiewashukuru watu” basi
pia nitoe shukrani zangu za dhati kwa Jumuiya ya Fii-sabilillah Tabligh Markaz
na wale wote waliochangia kwa hali na mali katika kuifanikisha maandalizi ya
uzinduzi wa Ijitimai hii. Wananchi wa Fuoni wanatambua na kuthamini juhudi kubwa kabisa walizozichukuwa maamiri
katika kuandaa mkusanyiko huu kwa kuitekeleza aya isemayo “nia ya kheri na kuamrisha mema na kukataza maovu…” Ala Imran aya ya
104. Aidha niseme asanteni sana kwa kunialika ili kujumuika nanyi leo hii katika kheri hii. Namuomba Mwenyezi Mungu
atutakabalie na aiweke juhudi hii katika mizani ya mema yetu- Amin.
Lengo
kubwa la Ijitimai ni kukumbushana mambo
ya kheri, kuamrishana mema na kukatazana maovu. Na hii ndio sababu iliyopelekea
umma wetu huu wa Mtume Muhammad (SAW) kuwa ni bora zaidi kuliko wote waliokuja
kabla yetu kama alivyosema Mwenyezi kwamba ‘’Hakika ninyi ni Umma bora, mumeletwa ninyi kwa ajili watu, naamrishana
mema na mnakatazana maovu na mnamuamini Mwenyezi Mungu”. Al-Imraan aya 110. Pia mkusanyiko huu wenye
waumini kutoka pande mbali mbali ni fursa nzuri ya kuelewana, kujenga umoja na
mshikamano, na kushauriana katika kutafuta mbinu za kujiletea maendeleo ya dini
na dunia yetu.
Ndugu
zangu katika imani,
Taasisi
zetu za dini zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika nchi yetu hii, Sote ni
mashahidi namna viongozi wa dini walivyoshikamana katika kuunganisha jamii hasa
pale jamii yetu ilipofarakana kwa sababu za kisiasa. Aidha tunashuhudia kazi
kubwa inayofanywa na mashekhe, maduati, maulamaa na taasisi za dini katika
kuelimisha umma, kujenga tabia na maadili mema, kuhimiza uadilifu na
uwajibikaji.
Ndugu Waislamu na ndugu Wananchi,
kazi ya kulingania ni shughuli yetu sote, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kujituma
kwa mujibu wa uwezo wake aliojaaliwa na Allah (SW). Hata hivyo hatuna budi kutambua kuwa kazi hii
ina miiko na maadili yake (Lingania
katika njia ya Mola wako kwa hekma na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa
namna njema zaidi). An-Nahli aya ya 125. Hekma ina maana kubwa lakini kwa
wepesi kabisa tunaweza kusema kuwa ni kukiweka kila kitu katika pahala pake
panapostahiki. Hivyo katika ulinganio wetu tuangalie mahitaji yetu na shida zinazotukabili
ili tuweze kuisaidia jamii yetu katika changamoto inazokabiliana nazo na kuleta
maendeleo. Iwapo maadili na miiko hii haitofuatwa, mlinganiaji anaweza kubomoa
badala ya kujenga na akaleta madhara makubwa badala ya kuinufaisha jamii. Na kama tunavyofahamu, sasa Nchi yetu inakabiliwa
na masuala mawili muhimu, moja ni:-
Ø mchakato
wa kurekebisha Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi niwaombe masheikhe
wetu, walimu wote, na Maaulamma , tuwaaidhi watu katika hali ya Amani na
Utulivu, ili kujenga mustakbali mwema katika nchi yetu. Kwani Mwenyezi Mungu
anatuhimiza kushikamana kwa kusema “Shikamaneni
katika kamba ya Mwenyezi Mungu na wala msifarikiane” Aya ya 103 Al-Imran.
Ø suala
la pili ni zoezi zima la kuhesabu watu (Sensa ya Watu na Maakazi), zoezi ambalo
linatarajiwa kufanyika kuanzia usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe 26-agosti
2012.
Ni
dhahir kuwa mpangilio wa masuala ya kuwapelekea maendeleo wananchi wake, katika
Nchi yoyote ile duniani si rahisi kufanyika kwa ufanisi kama Nchi hiyo
haitokuwa na uhakika wa idadi ya wananchi wake. Sote tunakumbuka kuwa kwa mara
ya mwisho watu walipohesabiwa ni karibu miaka kumi iliyopita, na sote ni
mashahidi ya jinsi tulivyoongezeka na jinsi huduma zinavyoonekana
hazitoshelezi. Kwa mfano, hivi sasa tunaambiwa kutokana na makisio tu, inakadiriwa
kuwa Zanzibar tuko watu karibu 1,200,000 lakini kwa kuangalia na kwa hesabu za
harakaharaka, wako wanaosema kuwa tuko zaidi ya hesabu hiyo. Lakini ukweli ni
pale tunapoona kuwa huduma kama za hospitali, maskulini, na masuala mengine
kama kuwafikishia umeme na maji wananchi tunavyoona, pamoja na jitihada zote za
Serikali yetu,lakini bado huduma hizo hazitoshi.
Hivyo
ni wajibu wetu kuwaelimisha jamiii umuhimu wa kutoa mashirikiano kadri
itakavytakiwa katika kuhakikisha mpango huu muhimu kwa Nchi yetu unafanikiwa
kwa manufaa yetu, Nchi yetu na Taifa kwa jumla.
Ndugu Waislam ,
Sisi
waumuni tumezunguukwa na nur kila pembe ya maisha yetu ‘Allah Nur, Wa Muhammad Nur, Wal
Quran.
Ndugu waislam na ndugu
wananchi,
Masheikh
na Tull-Ibul-ilmi, hivi sasa tunaishi katika ulimwengu uliopiga hatua kubwa
katika nyanja za habari na mawasialiano.
Kwa vile na sisi ni sehemu ya dunia, tujifunze na tuyatumie maendeleo
hayo na faida zake kwa kujiletea manufaa ya kidunia na akhera, hata hivyo tusije
tukasahau kuwa dini yetu imetuwekea dira ya kufuata tunaposikia habari
yoyote. Tusiwe na pupa, jazba, wala
tusiwe wepesi wa kushawishika; bali tunaposikia chochote tupime na
kuthibitisha.
Ndugu Waislamu,
nakuombeni tuitumieni fursa yetu ya kukutana pamoja kwenye Ijitimai hii kwa
kutafakari matatizo yanayozikabili jamii zetu na kutafuta mbinu muwafaka za
kiimani zitakazotusaidia kuondosha au kupunguza matatizo hayo. Tutumieni muda
wetu kushauriana juu ya hayo na kutafuta njia muwafaka ya kupambana nayo kwa
mbinu bora tulizofundishwa na dini yetu. Tunasihiane wala tusitukanane,
tujadiliane wala tusishindane kwa uadui, tuombeane kheri na uongofu wala
tusilaaniane na kuhukumiana ukafiri au unafiki. Mwenyezi Mungu pekee ndie
amjuae mchamungu na ndio ajuae yaliyofichwa vifuani mwetu. Wajibu wa muislamu
ni kulingania tu na hidaya inatoka kwake Mwenyezi Mungu. Tufuate mwenendo wa
Mtume wetu ambae pamoja na udhia mkubwa alioupata kutoka kwa Makureish hakukata
tamaa kuwalingania kwa kila njia na kuwaombea kwa kusema “Mola wangu wasamehe kaumu yangu bila shaka wao hawatambuwi”. Na sote tunaelewa historia yake ilivyoanza
mpaka akapata ushindi mkubwa na watu wakawa wanaingia katika dini makundi kwa
makundi.
Ndugu Waislamu,
katika Ijitimai hii tutapata fursa ya kuwasikiliza masheikh, wanavyuoni na
walinganiaji mbali mbali na kutoka sehemu tofauti. Tukumbuke kuwa lengo sio kusikia tu, bali
kinachotakiwa ni kufuata. Hivyo kila
mmoja wetu aweke azma kuwa atayatumia mafunzo atakayoyapata hapa katika maisha
yake yote. Atazidi kuyatekeleza yale
mazuri aliyonayo, atayawacha mabaya yaliyokatazwa, atadumisha mashirikiano na
wenzake, atajipamba kwa subira na atatenga baadhi ya muda wake kwa kujifunza zaidi. Ni matumaini yangu basi tukitoka hapa
tutakuwa tumetengeneza vyema imani zetu.
Lakini
kabla ya kumalizia naomba pia nichukue fursa hii kutoa wito kwa waislaam wote
kuichangia kwa hali na mali, si lazima kikubwa, hata kidogo ulichonacho, kwani
mbele ya Mwenyezi Mungu hakuna kidogo, ili Ijitimai yetu hii iweze kufanikiwa
na Inshaallah malipo yake tutayakuta kwa Allah (SW).
Mwisho
namuomba Mwenyezi Mungu aujaalie mkusanyiko huu uwe wa kheri, fanaka na faida
nyingi, vile vile tumuombe Mwenyezi Mungu atujaalie Matayarisho ya Katiba Mpya
yawe ya Amani na tulivu katika Nchi yetu. Pia ninawakaribisha wageni wote
waliotoka sehemu mbali mbali za Tanzania na nje ya Tanzania wajione kuwa wapo
nyumbani kwa kuwa Jimbo hili la Fuoni
limepata bahati kubwa ya kuwa na wageni wa namna hii basi tuwakirimu wageni
wetu kwa njia nzuri na ninaamini kwamba kuwepo
kwao sisi tutafarajika zaidi na ninaishukuru tena Jumuiya ya Fiisabilillah
Tabligh Markaz na wote waliofanikisha mkusanyiko huu.
“SASA
NAOMBA NITAMKE KUWA IJITIMAI YA KIMATAIFA YA MWAKA 2012, MARKAZI FUONI KUANZIA
TAREHE 6-8 JULAI
IMEZINDULIWA
RASMI”
Wabillah Tawfiq
Ahsanteni sana
No comments:
Post a Comment