SEMINA YA
VIONGOZI WA KIDINI JUU YA MAENDELEO YA UTALII NA MUELEKEO WAKE KATIKA KUKUZA
DHANA YA UTALII KWA WOTE
HOTELI YA
BWAWANI - TAREHE 18 JUNI 2012
MUWASILISHAJI
: ALI KHALIL MIRZA - MKURUGENZI MKUU KAMISHENI YA UTALII - ZANZIBAR
Yaliyomo
•
Maana ya Utalii
Aina za Utalii
Historia Fupi ya Utalii Zanzibar
Utalii kabla Mapinduzi
Utalii baada ya Mapinduzi
Kwanini Utalii?
Dhana za kuendeleza Utalii
•
Hali
halisi ya Utalii
•
Utalii
na Utamaduni
•
Utalii
katika nchi mbali mbali
•
Faida
ya dhana ya Utalii kwa wote
•
Muelekeo
TUNAMAANISHA NINI TUNAPOSEMA UTALII?
•
Utalii
ni kwenda kutembelea na kusoma nchi namna ya maumbile yake kijogorafia
•
Pia
kusoma tabia, desturi, utamaduni, miko, tambiko na historia ya nchi ile
Aina
za Utalii
•
Utalii
wa mapumziko (holidays)
•
Utalii
kibiashara
•
Utalii
wa mikutano
•
Utalii
wa kidini
•
Utalii
wa utamaduni na historia
•
Utalii
wa kimazingira(eco tourism)
HISTORIA FUPI YA UTALII ZANZIBAR
•
Zanzibar
ilisogezwa karibu na Ulaya mwaka wa 1869 baada ya kufunguliwa Suez Canal.
•
Baadae
kuanzishwa kwa Kampuni ya meli ya Kiingereza (British Indian Steam Navigation
Company) ambayo ilikuwa ikileta meli kila mwezi kupitia Aden mnamo mwaka wa
1872.
•
Kuanzishwa
kwa kampuni ya simu (Eastern Telegraph Company mwaka 1879) na kulazwa waya wa
simu baharini kutoka Zanzibar
•
Sultan
Khalifa bin Said kutangaza rasmi kuwa mtu ye yote atakayeingia Zanzibar ni mtu
huru katika mwaka wa 1889.
•
Uhusiano
wa karibu baina ya Zanzibar na Umarekani wa bishara wa wakati ule hasa baina ya
Zanzibar na Connectcut, Massachusetts na
Salem huko Boston.
•
Meli
kama vile Laurel chini ya nahodha Lovett ambayo ilianza safari yake ya
kwanza hapa Zanzibar tarehe 20 July, 1825 na baadae ikawa inakuja kila mwaka.
•
Kufuatia
na meli ya Ann chini ya nahodha Charles Millet mwaka wa 1826.
•
Kufutwa
kwa biashara ya Utumwa na Sultan
Barghash 1873
•
Uingereza,
Marekani na Ujerumani kuitambua rasmi Zanzibar
UTALII WA KALE
•
Hakukuwa
na Idara au Mamlaka ya Serikali kwa wakati ule iliyohusika na Utalii ila
kulikuwa na Kamati ya Utalii chini ya Resident wa Uingereza.
•
Kulikuwa
na kampuni binafsi zilizohusika na Utalii.
–
Leslie
and Anderson (East Africa) Ltd.
–
R.
Damador Bhimji & Company
–
Zanzibar
Tours and Holidays
BAADA YA MAPINDUZI
•
Baada
ya Mapinduzi Serikali iliendeleza dhana ya Umoja wa Mataifa ya wakati ule ya kuwa
utalii utumike kwa kukuza urafiki baina ya mataifa.
•
Ikaanzisha Shirika la Urafiki la Utalii ( Tanzania
Friendship Tourist Bureau, TFTB)
KWA NINI UTALII ZANZIBAR
•
Baada
ya kufikia miaka ya 80 Zanzibar ilitoka katika mfumo wa uchumi wa kijamaa na
kuweka hali maridhawa ya uwekezaji kutoka nje.
•
Hii
ilitokana na hali halisi ya ulimwengu ya wakati ule na pia kuanguka kwa zao la
karafuu.
•
Serikali
ikatunga Sheria ya Uwekezaji na kuanzisha Zanzibar Investment Committee (ZIC).
•
Kuanzishwa
kwa Mamlaka ya Uwekezaji 1986
•
Kuanzishwa
kwa Kamisheni ya Utalii 1992
•
Kuanzishwa
kwa Chuo cha Utalii Maruhubi 1992
DHANA MBALI MBALI ZA KUENDELEZA
SEKTA YA UTALII
•
Utalii unaweza kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa na
juhudi za kuongeza kipato cha watu (UNWTO)
•
Utalii pia
unasaidia juhudi za kuleta maendeleo endelevu (Benki ya Dunia)
•
Kwa nchi zenye uchumi duni na zinazoendelea utalii ni
sekta kichocheo kwa ukuaji wa sekta nyengine za kibiashara pamoja na miundo
mbinu (Umoja wa Mataifa)
•
Utalii unaweza kukuza uchumi ukiwekewa mikakati ya
kusaidia ukuwaji wa sekta yenyewe (OIC)
MAENDELEO YA SEKTA YA UTALII
•
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mpango Mkuu
wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini(MKUZA) umebainisha Sekta za Utalii na
Biashara ndio sekta viongozi kwa uchumi wa Zanzibar na hivyo kuahidi kutilia
mkazo katika maendeleo ya sekta hizo.
•
Halikadhalika Dira ya Maendeleo 2020 nayo pia imeipa kipaumbele Utalii kwa
kuongeza pato na kupunguza umasikini
HALI HALISI YA UTALII
•
Utalii unachangia asilimia 27 ya pato la taifa (GDP)
•
Unachangia asilimia 80 ya fedha za kigeni (foreign
exchange earnings)
•
Unatoa ajira za moja kwa moja kwa zaidi ya watu 12,500
na wengine 45,000 wanafaidika na sekta hii kwa njia isiyo kuwa ya moja kwa moja
(indirect & induced activities).
JE NCHI
INAWEZA KUENDELEZA UTALII NA KUDUMISHA MILA NA UTAMADUNI WAKE?.
Ni wazi kuwa utalii
ukitumika vizuri unaweza kutusaidia
kufikia malengo yaliyokusudiwa
•
Kama
tulivyotangulia kusema miongoni mwa vivutio vya utalii ni utamaduni.
•
Watalii
huenda kujifunza mambo waliyokuwa hawayajui
•
Kwa
hivyo utalii mahala pengi duniani unatumika kama njia ya kuhifadhi, kuenzi na
kutunza utamaduni wa nchi.
JE KUNA UMUHIMU KWA NCHI KUENDELEZA UTALII?
•
Kwa sababu za kiuchumi sio tatizo kwa nchi
kama Zanzibar kuendeleza Utalii kama ilivyo Afrika ya Kaskazini, Mashariki ya
Kati, Indonesia, Malaysia, Uturuki na kwengineko.
•
Mbali na sababu za kiuchumi na mazingira
utalii unaweza kutumika kukuza dini, maelewano, mila na silka zetu. Nchi kama Malaysia, hivi sasa ni mfano mzuri maendeleo ya aina
hiyo.
DHANA YA UTALII KWA WOTE
•
Utalii kwa wote unalenga zaidi kwa jamii kufaidika
kiuchumi na utalii
•
Jamii iweze kuainisha na kufanyia tafiti ili kupata historia halisi ya vivutio vya
utalii ikiwa ni maeneo ya asili, utamaduni, michezo na huduma.
•
Jamii iweze kuibua na kusimamia bidhaa ambazo
zitaingia katika soko la ndani la utalii (Branding)
•
Kuwa wabunifu kwa kuangalia vivutio vipya vya utalii
vinavyochunga maadili yetu. Mfano kivazi, lugha ,uvuvi, kilimo na taaluma
•
Ili tuwe na uwezo wa kuutumia utalii ili usilete
madhara ni kila mmoja wetu ashiriki katika sekta ya utalii akiwa katika
mazingira yake,
•
Nchi nyingi za Mashariki ya Mbali, Visiwa kama
Shelisheli, Mauritius, Maldives vimefanikiwa baada ya wananchi wake kushiriki
kikamilifu na kuwa na usemi mmoja kuhusu utalii.
MAZINGIRA BORA KATIKA KUFANIKISHA UTALII KWA WOTE
Katika kufanikisha Utalii uwe na Faida kwa Jamii yote ni muhimu:
-
Kila mmoja wetu awe na uwezo wa kushiriki na
kuzungumzia utalii
-
Taasisi na watu
binafsi wawajibike katika sehemu zao za kazi au maisha ikiwezo kudumisha usafi,
upatikanaji wa huduma nzuri, ukarimu, kutoa msaada wakati wa dharura, ulinzi wa watalii na mali zao, kutoa
maelekezo sahihi, kuthamini utamaduni wetu , uaminifu nk
MAZINGIRA BORA…..
Wawekezaji wahakikishe wanawekeza pia kujenga ujuzi na
uwezo wa wenyeji ili kupatikane wataalamu wa ndani ya nchi
•
Kwa ufupi maelezo hayo na miongozo ya
kitaifa na jumuia za mataifa tukiyafuata tutafanikiwa kukuza utalii, kukuza jina
la nchi yetu kiuchumi na kiutamaduni na kufanikiwa.
No comments:
Post a Comment