Na Salama Njani
Imeelezwa kuwa Tanzania
inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundo mbinu inayokidhi haja kwa watu wenye
ulemavu katika maeneo au majengo mbali
mbali ya huduma muhimu za jamii.
Mkurugenzi mkuu wa
ofisi ya taifa ya takwimu Dk Albina Chuwa, amesema kutokana na tatizo hili
zoezi la sensa ya watu na makazi ya mwaka huu imetoa kipaumbele kwa maswali
yanayohusu ulemavu ili kuisaidai Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa watu
wenye ulemavu ikiwemo miundo mbinu.
Amesema sambamba na
hilo madhumuni makuu ya kutoa kipaumbele kwa maswali ya ulemavu, ni serikali
kutaka kujua hali halisi na matatizo ya ulemavu pia kujua iwapo kama kuna aina
nyengine ya ulemavu ndani ya jamii.
Amesema Serikali inaelewa umuhimu wa watu wenye ulemavu na wanahaki ya kupata huduma zote za msingi kwa
kuwawekea miundo mbinu inayofaa, pamoja na kuwajengea mstakbali wa maendeleo
yao.
Dk Chuwa amewataka
wananchi wote kuwa tayari kutoa taarifa zao au za familia zao zikiwemo za watu
wenye ulemavu wakati wa zeozi la kuhesabu watu la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika kuanzia agosti 26 hadi
september 1 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment