Habari za Punde

Wiki ya Aggrey Morris - Afunga Ndoa Akwaa tuzo ya Mchezaji bora

Aggrey Thomas ametulia na kifaa chake kipya Mwanadada Asteria Thomas Mwashokela baada ya kufunga pingu za maisha tarehe 10 June 2012

Siku Aggrey Morris Alipofunga ndoa na Asteria Thomas Mwashokela katika Kanisa la Minara miwili  
Mhariri Mkuu Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC Omar Said Ameir akikabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Tanzania katika soka Aggrey Morris katika hafla hiyo.

Nadhani ni mwezi au wiki ambayo hatoisahau maishani mwake Big Up na hongera kwa kutuonesha njia hasa wachezaji wanaochipukia ambao wakiona mafanikio kama yenu huingiwa na morali wa kuzidisha juhudi nao wafanikiwe.

Aggrey Morris ni mchezaji wa Zanzibar Heroes, Taifa Stars na anakipiga timu ya Azam kwa sasa kama beki wa kati (Centre half).

Hivi sasa yupo na Timu ya Taifa ya Tanzania huko Msumbiji ambapo Stars watavaana na Mambas wikiendi

1 comment:

  1. Hongera zake!..mcheza kwao hutunzwa, nimependa namna harusi yake alivyokuja kuifungia nyumbani.

    Kila la kheri ktk maisha mmapya!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.