Na Salum Vuai, Maelezo
BAADA ya kuongozwa na viongozi wa kujishikiza kwa zaidi ya miongo miwili kwa kutokuendesha uchaguzi, hatimaye klabu kongwe ya soka hapa Zanzibar Miembeni, inatarajia kufanya uchaguzi Jumapili ya Julai 8, mwaka huu saa 3:00 asubuhi.
Zoezi la kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, lililoanza Jumatatu wiki hii, linafikia tamati leo, ambao kesho zitapitiwa ili kamati ya uchaguzi ijiridhishe na sifa za wagombea watakaojitokeza.
Msemaji wa klabu hiyo Sadi Justin, ameliambia gazeti hili kuwa, nafasi mbalimbali zitagombewa, ambazo ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Msaidizi wake, Mshika Fedha, Msaidizi wa nafasi hiyo pamoja na wajumbe kumi.
Hata hivyo, amefahamisha kuwa, kwa vile uongozi uliokuwwa ukiisimamia timu hiyo haujafanya uhakiki wa wanachama kwa kipindi kirefu, klabu hiyo inatoa wito kwa wote wanaojifahamu kuwa ni wanachama na hata wapenzi wa Miembeni kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi utakaokuwa kwenye jengo la klabu hiyo ili wajiorodheshe na kupiga kura.
Huku leo ikiwa siku ya mwisho kuchukua na kurejesha fomu, ni nafasi ya Mwenyekiti, Makamu na Msaidizi Katibu tu ndizo ambazo mtu mmoja kwa kila kiti amejitokrza kuchukua fomu.
Nafasi ya Mshika Fedha, Katibu Mkuu na wajumbe, bado hazijapata wagombea.
Justin ametoa wito kwa wanachama na wapenzi wa Miembeni kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo aliosema maandalizi yake yanasimamiwa na Katibu wa sasa Khamis Mussa..
Kutokana na kuingia kwenye mikono tafauti ya uongozi kila baada ya muda, klabu ya Miembeni iliyokuwa na jina kubwa hapa nchini, imekumbwa na mivutano ya mara kwa mara ambapo miezi kadhaa iliyopita, makundi ya vijana wanaojiita wapenzi wa timu hiyo, wameripotiwa kuwashambulia baadhi ya viongozi wakidai warejeshewe
No comments:
Post a Comment