Habari za Punde

Mama Mwanamwema Awatembelea Wazee wa Limbani na Kutowa Futari kwa Ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Wazee hao.

  MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Pemba alipofika kuwatembelea Wazee wa Limbani Wete na kutowa Futari kwa Wazee hao jana.
 Wazee wanaoishi katika  Nyumba ya Wazee Limbani Wilaya ya Wete wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipofika kuwatembelea na kutowa futari kwa ajili ya Mwezi  mtukufu wa Ramadhani jana 30-7-2012
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wazee wa Nyumba ya Wazee Limbani Wete Pemba alipofika kuwatembelea na kutowa futari kwa Wazee hao.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi futari Mzee wa Nyumba ya Wazee Limbani Hamadi Ali, wakati alipofika katika makazi yao kuwatembelea na kutowa  Futari kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati) Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawanke na Watoto Bi Zainab Omar

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akizungumza na Wazee wa Nyumba ya Wazee Limbani Wilaya ya Wete Pemba alipofika kuwasalimia na kutowa Futari kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.