Habari za Punde

Rais Kikwete Ahudhuria mazishi ya shemeji yake Lindi



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Jakaya  Mrisho Kikwete, amewasili mjini Lindi leo, Jumatatu,  Julai 30, 2012 kwa ziara ya siku mbili ambako miongoni mwa mambo mengine atafuturisha wananchi na viongozi wa mkoa wa Lindi.

Aidha, rais Kikwete amehudhuria mazishi ya shemeji yake , Marehemu Amani Kinyozi, aliyefariki siku ya Jumamosi jijini  Dar es salaam.


Rais Kikwete, ambaye ameongozana na mke wake Mama Salma Kikwete, alijumuika na mamia ya wakazi wa mji wa Lindi kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Mitandi, mjini humo.

Marehemu Amani Kinyozi, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 45, ameacha mke na watoto wawili.

Enzi za uhai wake marehemu alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mifuko ya karatasi, na pia  alikuwa akifundisha kinamama wajasiriamali ufundi huo katika juhudi za kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki, maarufu kama mifuko ya rambo ya kufungia bidhaa.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.
30 Julai, 2012          

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.