MFUKO wa huduma za jamii kwa wastaafu (PSPF), imewataka wanachama wake kuhakiki taarifa zao kila baada ya miezi mitatu ili kuweza kurekebisha jambo litakalo waondolea usumbufu wa kufuatilia mafao yao pindi wanapofikia muda wa kustaafu.
Kaimu ofisa mahusiano wa PSPF, Hawa Kikeke katika maonyesho ya 36 ya biashara kimataifa ambapo aliwataka wastaafu kutosubiri mpaka watakapo sumbuliwa.
Alibainisha kuwa uhakiki unafanyika ili kuhakikisha kama wanachama wote ni sawa na wapo hai, ambapo uhakiki mara nyingi hufanyika mwezi wa Januari na Julai, ambapo ukaguzi huo ni katika kuhakikisha usalama wa taarifa za mstaafu.
Alisema mara nyingi wamekuwa wakipokea malalamiko ya kutoendelea kuwajali wajane walioachwa na wastaafu hivyo wananchi wanapaswa kufahamu kuwa mjane anayetunzwa na mfuko huo ni yule ambaye mume au mke alikuwa mwanacha wa mfuko huo ambaye alifariki kabla ya muda wa kustaafu.
"Tungependa wananchi wafahamu namna mafao ya PSPF yanavyotolewa ili kuepukana usumbufu ambao umekuwa ukiwakanganya watu wafanyakazi ambao wanafariki kabla ya kustaafu wajane wao huendelea kupata pensheni yake
mpaka kifo, lakini kama mstaafu atakuwa amekwisha staafu na kupokea malipo yake mkataba wa PSPF na mstaafu huisha pale anapofariki na kamwe mafao hayo hayawahusishi ndugu wala watoto wa muhusika”, alisema Kikeke.
Aidha alisema PSPF imeandaa mkopo wa nyumba wa bei nafuu ambapo wanachama watakopeshwa kulingana na mahitaji yao, aidha nyumba hizo zitalipwa kutoka katika benki mbalimbali ambazo zitakuwa tayari zimeingia mkataba na ofisi ya PSPF.
“PSPF imejenga nyumba 640 katika mikoa mbalimbali hapa nchini, nyumba hizi zitawasaidia wanachama hasa wale wasiyo na nyumba katika jiji la Dar es Salaam nyumba hizo ziko maeneo ya Chanika, ambapo nyingine ziko katika mikoa ya Tabora, Mtwara na maeneo mengine”, alisema Kikeke.
Alisema nyumba hizo zitakopeshwa kwa watu ambao wameshachangia mchango kuanzia mitano na kuendelea ambapo hivyo wanachama wachangamkie huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment