Na Salum Vuai, MAELEZO
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar,
inajipanga kuhakikisha inatekeleza maazimio yaliyopitishwa katika mkutano wa
maendeleo endelevu (Rio+20), uliofanyika jijini Rio de Janeiro, Brazil Juni 20
hadi 22 mwaka huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej aliyekuwemo kwenye ujumbe wa Tanzania,
alisema miongoni mwa mikakati hiyo, ni pamoja na kuimarisha utekelezaji wa
mipango iliyopo.
Akizungumzia malengo ya katika
mkutano huo uliojumuisha marais, viongozi wa serikali na mashirika ya kimataifa
waziri huyo alisema mafanikio katika utekelezaji wa maazimio ya Rio ya mwaka 1992 yatafanyiwa tathmini na kutambua
mapungufu yaliyojitokeza katika utekelezaji wake.
Alisema ni kupata ridhaa ya
kisiasa ya kuendelea kuimarisha utekelezaji wa maazimio ya mwaka 1992, na
kutambua changamoto zinazokwamisha utekelezaji wake na kupanga hatua za baadae.
Aidha, mkutano huo umebaini kuwa, dunia imeshuhudia kukosekana kwa uhakika wa chakula, njaa, upungufu wa maji, kuongezeka kwa umasikini, ukataji ovyo wa miti, matatizo mbalimbali ya kijamii, ukosefu wa ajira na kuanguka kwa uchumi wa dunia.
Hata hivyo, Ferej alisema pamoja
na changamoto hizo, Tanzania
ilishiriki mkutano huo ikiwa imepata mafanikio mbalimbali katika utekelezaji wa
azimio la Rio la mwaka 1992, ikiwemo uundwaji
wa taasisi tafauti, sera na sheria zinazosimamia shughuli za mazingira.
Alitoa mfano kwa upande wa
Zanzibar kuanzishwa kwa Idara ya Mazingira mwaka 1989 kabla ya azimio la Rio
1992, ambapo imemudu kuanzisha sera ya mazingira ya 1992 na sheria ya mazingira
ya mwaka 1996, kutayarishwa kwa dira ya maendeleo 2020, mkakati wa kukuza
uchumi na kupunguza umasikini (Mkuza I na II-2000/05 na
2010/2015).
Alifafanua kuwa malengo hayo
yanaelekea zaidi katika azma ya kuongeza ajira, matumizi endelevu ya rasilimali
za bahari na maandalizi makini ya kukabiliana na majanga, mafuriko na ukame.
Waziri huyo alisema mipango ya Zanzibar katika kutekeleza
maazimio hayo, ni kuimarisha uwezeshaji wa sekta mbalimbali pamoja na wananchi,
ukuaji wa teknolojia, upatikanaji wa vitendea kazi na fedha.
Aidha alieleza kuwa, serikali itaendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo na wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa ikiwemo UNDP, UNEP, FAO na mengineyo katika kutafuta vyanzo mbalimbali vya rasilimali zitakazosaidia kuimarisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aliahidi kuwa, serikali itaimarisha usimamizi wa
rasilimali zitakazotumika wakati wa utekelezaji wa maamuzi ya mkutano huo ili
kuhakikisha uthamani wa fedha zinazotolewa na washirika wa maendeleo ili
kuongeza imani kwa washirika hao na wananc
No comments:
Post a Comment