Habari za Punde

Mwandishi Ahmed Rajab, MCT wakutana na Mwenyekiti tume ya mabadiliko ya katiba

 Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw. Neville Meena (kulia) akiongea katika mkutano wa kubadilishana mawazo na uongozi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana (Jumanne, Agosti 13, 2012).
 Waandishi wa Habari Wakongwe, Bi. Pili Mtambalike (kulia), Bw. Allan Lawa (katikati) na Bw. Suleiman Seif wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba, akiongea na Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana (Jumanne, Agosti 14, 2012) (Picha na Tume ya Katiba)

  Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kati ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba na Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana (Jumanne, Agosti 14, 2012).(Picha na Tume ya Katiba)
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba (katikati) akimtambulisha Mwandishi wa Habari Mkongwe, Bw. Ahmed Rajab (wa pili kushoto) kwa Wajumbe wa Tume. Kulia ni makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na kushoto ni Mjumbe wa Tume, Dkt. salim Ahmed Salim (kushoto) na Katibu wa Tume, Bw. Rashid Assaa. Bw. Rajab alikutana na Wajumbe wa Tume kubadilishana mawazo katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana(Jumanne, Agosti 14, 2012). (Picha na Tume ya Katiba)
Mwenyekiti wa Tume ya Mabdiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba, akiongea na Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana (Jumanne, Agosti 14, 2012) kubadilishana mawazo. Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa MCT, Bw. Kajubi Mukajanga. Kulia ni Katibu wa Tume Bw. Rashid Assaaa.(Picha na Tume ya Katiba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.