Jengo laBwana Abdulla Ali Khamis ambalo limo ndani ya eneo la chuo cya Sayansi ya AfyaKilichopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Makamu waPili wa Rais wa ZanzibarBalozi Seif Ali Iddi akimpongeza mwanachama mpya aliyejiunga katika Jumuiya yawachangiaji damu kwa Hiari Zanzibar Bibi Maryam Mohd akichangia damu kwa maraya kwanza katika kituo cha damu salama Kiliopo Sebleni Mjini Zanzibar.
Jengo jipya la Bohari Kuu ya Wizara ya Afya linaloendelea kujengwa ndani ya eneo lakiliokuwa kiwanda cha Sigara Maruhubi Mtoni
Na Othman Khamis Ame
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anakusudia kumuandikia Barua Waziri anayesimamia masuala ya Ardhi Zanzibar kumtaka kufuta mara moja hati ya umiliki wa Viwanja vya nyumba ambavyo vimo ndani ya eneo la Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni.
Balozi Seif alitoa kamuli hiyo wakati akiangalia eneola Chuo hicho ambalo limevamiwa kwa ujenzi ndani ya ziara yake katika Taasisi zilizomo ndani ya Sekta ya Afya ikiwa ni mwanzo wa ziara zake kuangalia utendaji wa Wizara zaSerikali pamoja na changamoto zinazozikabili Wizara hizo.
Balozi Seif akionyeshwa kukasirishwa kwake na tabia yabaadhi ya watu kukaidi maamuzi ya Serikali pamoja na Maagizo ya Mahkama ya kuhodhi ardhi alisema Taifa halitakuwa na Maendeleo kama Jamii ikijali zaidi Ubinafsi.
Aliagiza kusitishwa mara moja maendeleo ya ujenzi wa nyumba moja ambayo tayari ina mgogoro ulioko mahakamani pamoja na kuzuiwa kwa ujenzi wowote kwa wale waliomilikishwa viwanja saba ndani ya eneo hilola chuo. “ Kamwe hatutaacha maendeleo ya Umma kwa kuachia Mtu au watu binafsi. Kwa Tabia hii hakuna namna ya kufanikisha Maendeleo ya chuo kama hakutakuwa na Ardhi”. Alitahadharisha Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali haikusudii kufanya ubabe kwa raia wake lakini kamwe haitasita kuchumchukulia hatua za kisheria Raia atakayeonyesha dharau au jeuri dhidi ya Serikali.
Alieleza kuwa haipendezi kuona Washirika na wafadhili wanaendelea kutoa misaada mbali mbali katika uendelezaji wa majengo na Taasisiza Serikali huku Viongozi wanasema kuna maeneo ya ujenzi wa Taasisi hizo.
Aliupongeza Uongozi wa Wizara ya Afya kupitia Chuo hicho kwa juhudi zake za kuendeleza Majengo yatakayokidhi mahitaji ya wanafunzikwa siku za baadae.
Mapema Msimamizi wa Ujenzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni Ndugu Waziri Juma alimueleza Balozi Seif kwamba Eneo hilo lilikuwa likimilikiwa kihalali na Chuo cha Ufundi cha Mbweni tokea mwaka 1962.
Ndugu Waziri Alisema Chuo cha Sayansi kikilazimika kisheria kuomba eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa chuo chake ambapo baadaye uongozi wa chuo hicho ukaamua kujenga ukuta baada ya kuanza dalili za uvamizi wa eneo hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitembelea Madarasa ya chuo hicho na kuridhika na hatua ya ufundishaji iliyofikiwa na uongozi wa chuo hicho.
Balozi Seif aliangalia shughuli za kila siku ya Maabara ya Kitengo cha Mapambano dhidi ya Maradhi ya Malaria kiliopo Mwanakwerekwe ambapo Meneja Mkuu wa Kitengo Hicho Bwana Mwinyi Mselemu alisema alieleza mkakati mpya wakuiweka Zanzibar huru na ugonjwa wa Malaria.
Alisema Utaratibu unaandaliwa wa kufuatilia kesi za wagonjwa wa malaria katika kila shehia kila baada ya wiki mbili kwa lengo la kufanikisha mkakati huo.
Baadaye Balozi Seif alikagua harakati za uchangiaji damu katika Kutoa cha kuchangia damu kiliopo Sebleni ambapo Meneja Mkuu wa Kituo hicho Dr. Mwanakheir Mahmoud alizitaja baadhi ya changamoto zilizopo ni kupungua kwa kasi ya wachangiaji damu.
Akiangalia ujenzi wa Bohari Kuu ya Wizara ya Afyailiyopo ndani ya iliyokuwa kiwanda cha sigara Maruhubi Balozi Seif alielezea kuridhika kwake na hatua hiyo ambayo italeta faraja kwa Wizara ya Serikali ya ujumla.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seifalimalizia ziara yake kwa kuangalia utendaji katika maabara za Hospitali kuu ya Mnazi mmoja pamoja na Bodi ya chakula , Dawa na Vipodozi.
Watendaji wa Taasisi hizo alisema zipo changamoto ambazo serikali kuu inastahiki kuzifanyia kazi zikiwemo baadhi ya mashine zinazohitaji vipuri ambavyo ni mzigo kugharamiwa na vitengo vyao.
Kwa Upande wake Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Bw. Burhan Othman Simai alisema yapo mafanikio makubwa kwa Taasisi yake katika mapambano dhidi ya wafanyabiashara wakorofi wanaoshindwa kufuata taratibu na sheria za Nchi.

.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment