Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Hui Liangyu baada mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana,akiwa katika ziara ya siku mbili. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Hui Liangyu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa katika ziara ya siku mbili ,Makamo Waziri Mkuu Liangyu akiwa na ujumbe wake walifanya mazungumzo na Rais [Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Othman,Ikulu.]
NA Rajab Mkasaba , Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Hui Liangyu huku China ikiahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta za maendeleo.
Katika mazungumzo hayo viongozi hao walieleza ni kwa namna gani nchi mbili hizo zimeweza kukuza na kuimarisha uhusiano huo wa muda mrefu ambao umeweza kuleta manufaa zaidi.
Aidha, Dk. Shein alimueleza Naibu Waziri Mkuu huyo kuwa Zanzibar inajivunia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na China ambao ulianzishwa na viongozi waasisi akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Mwenyekiti Mao Tse Dung.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa ipo haja ya kuimarisha uhusiano zaidi katika sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo, afya na miundombinu.
Dk. Shein pia, katika mazungumzo hayo alieleza haja ya kuanzishwa kwa kituo cha uchunguzi wa mambo ya kilimo ili kuimarisha kilimo hapa Zanzibar.
Dk. Shein pia, alimpongeza Serikali ya China kwa jitihada zake za kuleta wataalamu wa sekta mbali mbali hasa sekta ya afya ambao wameweza kufanya kazi vizuri na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Zanzibar.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Mhe. Liangyu kuwa uchumi wa Zanzibar umekuwa ikiimarika siku hadi siku na kueleza kuwa bado Zanzibar ina mengi ya kujifunza katika sekta hiyo kutoka nchi za China.
Dk. Shein pia, aliipongeza China kutokana na mradi wake maalum wa kupambana na umasikini katika nchi za Afrika na kueleza kuwa anaamini kwua Zanzibar itaendelea kufaidiaka na fursa zinazopatikana kutoka mradi huo.
Aidha, Dk. Shein alimuhakikishia kiongozi huyo kuwa Zanzibar ni salama na atafurahia ziara yake hiyo kwa muda wote akaokuwepo hapa.
Pia alimueleza kuwa mafanikio makubwa yamerweza kupatikana kutokana na kuwepo kwa mashirikiano mazuri ya uongozi chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.
Nae Mhe. Liangya alimueleza Dk. Shein kuwa China itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Zanzibar kwani ni uhusiano wa kihistoria kutokana na kuwa wa muda mrefu na wenye manufaa makubwa.
Kiongozi huyo pia, alisifu juhudi za Serikali ya Mapindyzi Zanzibar katika kuwaletea maendeleo wananchi na kueleza na kuahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika skta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta ya kilimo.
Kiongozi huyo aliahidi kuwa Serikali ya Chaina itaendelea kutoa ushirikiano katika maeneo mbali mbali ya kiuchumi yakiwemo yale yaliogusiwa na Mhe. Rais katika mazungumzo yao.
Kiongozi huyo alaieleza haja ya kuimarisha sekta ya kilimo kutokana na kuwa sekta hiyo ni muhimu katika kukidhi mahitaji ya chakula kwa wananchi ikiwa ni sekta muhimu kwa taifa lolote katika kuwapatia wananchi wake mahitaji hayo ya chakula.
Alieleza kuwa China imepiga hatua kubwa katika sekta hii na kusisitiza kuwa China itahakikisha inatumia uzoefu wake katika kuisaidia Zanzibar katika sekta hiyo. Aidha, kiongozi huyo alimuhakikishia Dk. Shein kuwa China itatoa ushirikiano wa kutosa katika uvuvi wa bahari kuu, mifugo, afya na sekta nyengine muhimu.
Kiongozi huyo pia, alimueleza Dk. Shein kuwa ujumbe na wataalamu aliofuatana nao utahakikisha kuwa kabla ya kuondoka unakutana na wataalamu na viongozi wa Zanzibar kwa lengo la kujadili zaidi jinsi ya kufanikisha masuala yaliozungumzwa na viongozi hao.
Pia, alieza kuwa Zanzibar ina mazingira mazuri na imebarikiwa na kuwa na rasilimali nyingi na anaamini kuwa Zanzibar itaendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo.
Mhe. Liangya yupo nchini kwa ziara ya siku tatu kama sehemu ya ziara ya nchi za Afrika ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao walisisitiza haja ya kuimarishwa zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo.
Wakati huo huo pia, katika kuendeleza ushirikiano wa kirafiki kati ya Zanzibar na Jamhuri ya Watu wa China, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimetiliana saini juu ya Mashirikiano ya Kiuchumi na Kiufundi ambapo Zanzibar imepatiwa jumla ya RmB 60 milioni sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 14.8.
Katika utiaji saini huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar baada ya mazungumzo hayo mbele ya Dk. Shein kwa upande wa Zanzibar alitia saini Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ambapo kwa upande wa China alitia saini Waziri Naibu Waziri wa Biashara Mhe. Zhong Shan ambapo ulishuhudiwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seid pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa China Bwana Hui Liangyu
Fedha hizo zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa majengo mapya na ukarabati mkubwa wa majengo yaliopo katika Hospitali ya Abdalla Mzee, ujenzi wa skuli ya msingi Mwanakwerekwe, utiaji wa taa za barabarani zitakazotumia nishati ya jua katika baadhi ya barabara kuu za Mjini.
Aidha, miradi mengine ni mafunzo mafupi na marefu katika fani mbali mbali ambazo yatapendekezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, uchimbaji wa visima vya maji pamoja na maeneo mengine yatakayokubaliwa na pande hiz.
Aidha, ujumbe huo umetiliana saini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar juu ya msaada wa Wataalamu wanne kutoka China ambao watakuwepo Zanzibar kwa muda wa miaka miwili.
Wataalamu hao watawafundisha mafundi wa Zanzibar wa mitambo na studio ya kurushia matangazo ya redio pamoja na kutoa vifaa mbali mbali kwa ajili ya studio hiyo.
Viongozi mbali mbali walihudhuria katika mazungumzo hayo wakiwemo Mawaziri , Makatibu na viongozi wengine kutoka Zanzibar ambapo kwa upande wa ujumbe wa kiongozi huyo aliambatana na Manaibu Waziri na viongozi wengine
No comments:
Post a Comment