Habari za Punde

Sheria na kanuni zinazohusiana na matumizi ya simu zipo - Naibu Mkurugenzi TCRA

 Naibu Mkurugenzi ambaye pia ni Mratibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania { TCRA } Kanda ya Dar es salaam Bwana Victor Nkya akiwasilisha mchango wa Maafa wa mamlaka hiyo wa Shilingi Milioni5,000,000/- kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapoOfisini kwake Vuga Mjini Zanzibar


MtakwimuMkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nd. Mohd Hafidh akitoa tathmini ya zoezi la sensa ya watu na Makazi lililomalizika mwishoni mwa Wiki iliyopita mbele ya Kamati ya Taifa ya Sensa Zanzibar. Kamati hiyo ya Taifa ya Sensa ilikutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika ukumbi wa Ofisi yake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

 Picha na Hassan Issa wa–OMPR- ZNZ.

Imeelezwa kwamba mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya matumizi mabaya ya simu iwe ya mkononi, majumbani na hata Maofisini ikiwemo matusi adhabu yake ni miezi sita Jela au Faini ya Shilingi milioni Tano au adhabu zote mbili.
 
Naibu Mkurugenzi ambae pia ni mratibu wa Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania{ TCRA } Kanda ya Dar es salaam Bwana Victor Nkya  alisema hayo wakati akizungumza na Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddihapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.


Bwana Nkya aliyeuongoza Ujumbe wa Viongozi wanne wa Mamlaka hiyo na kukabidhi mchango wa Shilingi Milioni 5,000,000/- kwa Mfuko wa Maafa Zanzibar kufuatia ajali ya M.V.Skagit miezi miwili iliyopita alisema sheria na kanuni zinazohusiana na matumizi ya Simu zipo.
 
Alisema licha ya asilimia 95% ya sim Card zotezinazotumika Nchini Tanzania kusajiliwa katika kampuni tofauti yanayoendesha biashara ya simu lakini badozipo hitilafu zinazopelekea baadhi ya watu kutumia vibaya fursa za matumizihayo ya simu.
 
“ Mtu atakayetumia Simu kinyume na taratibu zilizoainishwa katika sheria na kanuni zilizopo endapo atapatikana na hatia adhabu yake ni jela miezi sita au faini ya shilingi Milioni 5,000,000/-”. Alisisitiza Bwana Nkya.
 
Naibu Mkurugenzi huyo wa Malaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Dar es salaam alifahamisha kwamba Uongozi wao upo hapa Visiwani kuangalia mazingira ya namna ya Kufungua Ofisi yao Zanzibar.]
 
Alisema Mamlaka yao ambayo inahusiana na masuala ya Taasisiza Simu, Tv, Redio pamoja na Internet ina nia pia ya kuwa na kituo cha mtandaowa pamoja wa Internet Nchini kwa lengo la kurahisisha mawasiliano hayo.
 
Bwana Nkya alifahamisha kwamba hatua hiyo itakwenda samba mba na uimarishaji wa mawasiliano ya Mtandao wa Internet katika vyuoVikuu Nchini ambao utasaidia kumuwezesha mwanafunzi wa chuo Kikuu kujisomea kwakina  zaidi kupitia mitandao hiyo.
 
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania{ TCRA } kwa mchango wake huo uliokuja kufuatia maafa hayo ya kuzama kwa Meliya M.V.Skagit ambayo yataendelea kukumbukwa miaka kadhaa ijayo.
 
Balozi Seif alieleza kwamba kitendo chao hicho niishara ya muendelezo  wa Mila, Silka naUtamaduni wa Waafrika katika kufarijiana wakati wana jamii wenzao wanapopatwana misiba.
Wakati huo huo Kikao cha Taifa cha Sensa Zanzibar kimekutana mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uandikishaji wa sensa ya watu na Makazi lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Kikao hicho kilichoshirikisha Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Maafisa Tawala wao wa Mikoa na wilaya zote za Zanzibar kilifanyika chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 
Wajumbe wa kikao hicho wamekutana katika ukumbi wa Ofisiya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi uliopo Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
 
Akitoa tathmini ya zoezi hilola Sensa ya watu na makazi Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nd. Mohd Hafidh alisema asilimia 87.3 ya Kaya zote za Zanzibar zimehesabiwa baada ya wiki ya nyongeza ambapo awali ilikuwa Asilimia 82.4.
 
Ndugu Mohd Hafidh alivipongeza vikundi vya Polisi Jamii katika shehia mbali mbali Nchini kwa juhudi zao zilizopeleka kudumu kwa usalama katika kipindi cha zoezi hilo  licha ya kuwa na matukio ya wasi wasi kwa baadhi ya shehia hizo.
 
Hata hivyo Ndugu Hafidh alisema zipo changamoto zilizojitokeza katika zoezi hilo ambapo miongoni mwake zikiwa ni  pamoja na baadhi ya watu kususia zoezi hilo kwa visingizio vya migogoro ya Kijamii katika maeneo yao pamoja na  suala la upatikanaji wa Vitambulisho vya Mzanzibari

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.