Habari za Punde


YAH: TAMKO LA PPAT KULAANI KUSHAMBULIWA NA KUSABABISHA
 KIFO CHA MWAKILISHI CHANNEL TEN IRINGA DAUDI
Chama cha Wapiga picha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na jamii ya wanahabari nchini, watanzaniawote  kutoa pole kwa Familia ya Marehemu DaudMwangosi na KULAANI mauaji ya kikatili ya Mwandishi Daud Mwangosi wa ChannelTen mkoani Iringa.
 
Mwangosi ambaye pia alikuwa niMwenyekiti wa Klabu ya wanahabari Mkoani Iringa (IPS) alifikwa na umautiSeptemba 2, 2012 majira ya saa 10 jioni wakati wa vurugu za Polisi na Wafuasiwa CHADEMA.
 
PPAT inalaani kwa nguvu zotekitendo hicho cha kinyama na ambacho kimetishia kwa kiwango kikubwa usalama wawaandishi wa habari hasa Wapigapicha kama Mwangosi ambao hutakiwa kuwa mstariwa mbele katika kupiga picha za matukio mbalimbali.
 
Polisi ikiwa ni chombo pekeecha usalama wa raia na mali zao wakati wote ilishindwa kuhakikisha Mwandishi,Daud Mwangosi anakuwa salama na kutekeleza wajibu wake vyema.


Ni hao hao Polisi tumewaonakatika picha kadhaa wakimshambulia na hatimaye kutawanyika baada ya kufa kwaMwangosi lakini ajabu tunasikia kupitia taarifa zao kuwa Mwangosi alikuwawakati akikimbia kutoka upande wa Wananchi.
 
PPAT inapenda kutoa wito kwaMkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Said Mwema na kuwaajibisha Askari wotewaliohusika katika tukio lile akiwepo RPC wa mkoa wa Iringa na kisha yeyemwenyewe pia kuwajibika kutokana na mauaji hayo ya kinyama.
 
PPAT pia inaungana na vyama vyote vya Waandishi wahabari nchini Tanzania katika kutaka uchunguzi huru na wahaki ulio katika uwazikatika kuchunguza kifo cha Mwandishi Mwenzetu Daudi Mwangosi na majibu yakeyawekwe hadharani mapema iwezekanavyo .

Pia PPAT inawaunga mkono Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa (IPC)kuwazuia wanachama wake kuandika Habari zozote za Jeshi hilo Mkoani Iringa.PPAT inaomba vyama vyote vya mikoa na Jukwaa la Wahariri TEF kusitishauandikaji wa habari zozote zinazolihusu Jeshi la Polisi nchini hadi watakapowawajibisha waliotenda mauaji hayo.

Mroki Mroki
Katibu Mtendaji PPAT.
0717002303/0755 373999

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.