Na Nafisa
Madai
WMM
Wafanyakazi
wa kiwanja cha ndege Pemba wamesema mapato yanayopatika kiwanjani hapo hayakidhi mahitaji ya kiwanja
hivyo serikali kupitia wizara husika wanahitaji kutupia macho na nguvu zao kiwanjani hapo.
Wamesema
hayo wakati walipotembelea na waziri wa miundombinu na mawasiliano Mhe Rashid
Seif ambapo wamesema kwa vile sasa wanatakiwa kubadilika kiutendaji tokea
kuundwa kuwa mamlaka kamili serikali haina budi kuelekeza nguvu zao kiwanjani hapo
ili kukifanya kiwanja hicho kuwa na hadhi na haiba nzuri kwa wenyeji na wageni
wanaotumia kiwanja hicho.
Aidha
wamesema mpaka sasa hivi bado hawajaona mabadiliko yoyote tokea kundwa mamlaka
Jambo ambalo linarudisha nyuma ufanisi wa kazi zao.
Hata hivyo
wamesema bado kama mamlaka wanafanya kazi katika mazingira magumu sana hasa
pale wanapofanya upekuzi mizigo ya abiria hulazimika kutumia mikono na wala
hawafahamu mizigo ile kama ipo salama ama laa.
Wafanyakazi
hao wamemuomba waziri huyo kufanya juhudi za makusudi kutafuta mashine alau
moja ya kupimia mizigo ya abiria ili waweze kugundua ndani ya mizigo kuna kitu
gani.
Aidha
wamemtaka waziri huyo kuchukua hatua maalumu kwa gari zinazoingia ndani ya
kiwanja kwani wamesema kuna baadhi ya gari zinazokuja kuchukua viongozi huingia
ndani ya uwanja jambo ambalo limekuwa likiharibu barabara za ndege yaani(
apron).
Kwa upande
wake waziri Seif amesema lengo haswa la kufanya ziara katika taasisi mbali
mbali za wizara yake ni kuangalia mapungufu yaliyopo ili kuhakikisha mapungufu
hayo yanapatiwa ufumbuzi yakinifu.
Aidha Waziri
seif aliwatoa wasiwasi wafanyakazi hao kuwa hakuna tofauti katika ya kiwanja
cha ndege unguja na cha pemba hivyo alimtaka meneja msaidizi kuhakikiksha kuwa
hudma zinazotolewa unguja lazima
Pemba
ziwepo.
Sambamba na
hayo aliwataka wafanya kazi hao kubadilika katika utendaji wao na wawe wabunifu
ili waweze kujitangaza ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo uwanja wa ndege ni sehemu nzito ya
kufanya kazi ambapo alisema kila aliepewa dhamana ahakikishe anawajibika
ipasavyo kwa vile kazi ni sehemu ya maisha yao.
Baada ya
mazungumzo hayo mhe Waziri alitembelea jengo hilo kwa kukagua sehemu ya choo
ambavyo vimefanyiwa matengenezo, sehemu ya zima moto na kuangalia mnara wa
Zantel ambao upo karibu na eneo la kiwanja hicho.
No comments:
Post a Comment