Habari za Punde

Ripoti ya Kuzama kwa Meli ya MV Skagit Zanzibar.

 Katibu Mkuu Kiongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, akionesha ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa kuzama kwa Meli ya MV Skagit katika bahari ya Zanzibar ikitokea Dar-es- Salaam, ripoti hiyo tayari imeshakabidhiwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu Zanzibar. Katibu Mkuu Kiongozi amesema ripoti hiyo itakuwa katika Makumbusho ya Nyaraka za Kale Kilimani
 
 Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, akisoma ripoti ya Tume ya Kuchunguza kuzama kwa Meli ya MV Skagit Zanzibar ,kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali  vilioko Zanzibar, katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Weles.
 Waandishi wakiwa makini kuchukuwa habari ya ripoti ya Tume ya Kuchunguza kuzama kwa Meli ya MV Skagit katika bandari ya Zanzibar  


 Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la ZBC Redio Juma Abdalla akitaka ufafanuzi wa ripoti hiyo baada ya kusomwa mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Weles Zanzibar.
 Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Munir Zakaria  akiuliza swali katika mkutano huo wa kuwasilisha ripoti ya kuzama kwa meli ya MV Skagit.
 Mdau wa habari Mohammed Mhina akitaka ufafanuzi wa ripoti hiyo kwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kuwasilisha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilivyoko Zanzibar. 
 Mwandishi wa habari  wa Kituo cha ITV  Zanzibar Farouk Karim akuliza swali  kwa Katibu Mkuu Kiongozi baada ya kuisoma ripoti hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa kuwasilisha ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa kuzama kwa Meli ya MV Skagit, baada ya kuisoma ripoti hiyo mbele ya waandishi katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Weles 

1 comment:

  1. Maalim wangu ulinisomesha Chemistry, unaisoma ripoti iliyojaa majonzi na masikitiko huku unatabasamu?

    Ndio upo mbele ya waandishi wa habari lakini kuna roho zilipotea na ripoti hii ilisubiriwa angalau walioondokewa wapate angalau nafuu ya msiba mkubwa uliowapata hivyo tabasamu haikuwa mahala pake Maalim wangu kama utanisikiliza.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.