Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Tanzania Mhe. Joseph Sinde Warioba, akitowa maelezo kwa Wananchi kuhusu kuchangia Katiba ya Tanzania wakati wa Mkutano wa kutowa maoni yao kuhusu Katiba katika viwanja vya Ijitimai ya Zamazi mwenakwerekwe.
Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Tanzania Mhe. Joseph Sinde Warioba, akionesha Katiba ya Tanzania ambayo inatakiwa kufanyiwa marekebisho, wakati wa kutowa maoni ya yao mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Tanzania wakati wa Mkutano wa kutowa maoni yao kuhusu Katiba katika viwanja vya Ijitimai ya Zamazi mwenakwerekwe
Mwenyekiti wa Tume Mhe.Joseph Sinde Warioba,akiwa na Wajumbe wa Tume wakisikiliza maoni ya Wananchi wa Jimbo la Mwanakwerekwe wakitowa maoni yao mbale ya Tume katika viwanja vya Ijitimai ya Zamani Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mwananchi Saida Abdalla Mussa akitowa maoni yake mbele ya Tume kuhusu Marekebisho ya Katiba ya Tanzania.
Mwananchi Fauzia akitowa maoni yake na kutaka mitihani ya kidatu cha nne isiwe ya pamoja iwe kila upande na mitihani yake
Mwananchi mkaazi wa Mwanakwerekwe Ali Suleiman Shihata, akitowa maoni yake katika mkutano wa kutowa maoni ya marekebisho ya Katiba ya Tanzania uliofanyika katika viwanja vya Ijitimai Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mkaazi wa Mwanakwerekwe Unguja Juma Ali Khamis, akichangia maoni yake katika viwanja vya Mwanakwerekwe Unguja.
Wananchi wakiwa katika sehemu maalum ilioandaliwa kwa Wananchi wanaotaka kutowa maoni yao
Wananchi wa Mwanakwerekwe wakifuatilia utoaji wa maoni yao katika viwanja vya Mwanakwerekwe, wakati wajumbe wa Tume walipofika katika viwanja hivyo kukusanya maoni yao ya Marekebisho ya Katiba Tanzania.
Mwananchi Namani Mustafa akitowa maoni yake ya marekebisho ya Katiba ya Tanzania, katika viwanja vya mwanakwerekwe Unguja.
Kijana Hassan Haji Khamis akichangia maoni yake kutaka kutaka Zanzibar irejeshewe kiti chake katika FIFA.
No comments:
Post a Comment