Habari za Punde

CCM yawashtukia vishoka wa ajira

 
Na Mwandishi wetu
CHAMA cha Mapinduzi kimeelezea kusikitishwa na vitendo vya hadaa na utapeli vinavyofanywa na baadhi ya watu wachache kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa madai ya kuwapatia ajira vijana katika vyombo vya ulinzi na usalama nchini na maeneo mengine.
Aidha chama hicho kimelaani vitendo hivyo viovu na kusema endepo vikiachwa kuendelea vinaweza kuchafua haiba na taswira njema ya taifa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alitoa kauli hiyo Amani wakati akizungumza na vijana waliokumbwa na kadhia hiyo na kuongeza kuwa CCM haipo tayari kushirikiana wala kumlinda mwana CCM au mwananchi mwengine atakaeshiriki katika vitendo hivyo.
Alisema CCM na serikali kwa ujumla haitambui kuwepo kwa mipango kama hiyo ya kuwatoza fedha vijana ili wapatiwe ajira serikalini.
Alisema CCM kamwe haiwezi kukubali wala kuvumilia vitendo vya aina hiyo vya utapeli kuona vinaendelea kufanywa kwa vijana.
Aidha Naibu huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana walioathirika na mkasa huo kutoa kila aina ya mashirikiano na vyombo vya dola ili haki iweze kutendeka.
Pia ametoa tahadhari kwa vijana pamoja na wananchi wote kuwa waangalifu hasa katika kipindi hiki na wasikubali kuingizwa katika vitendo vya utapeli vinavyofanywa na watu wasiokuwa na imani wala utu mbele ya wenzao.

2 comments:

  1. Kwanza niekeni sawa hapa, kwani ajira inatolewa na ccm au Serekali ya SUK ndio yenye majukumu hayo?.
    Hii ndio hatari iliotukumba Wananchi wa Zanzibar kuiuza Dola ya Zanzibar Dodoma na tukachanganyishiwa kokteli.

    Tatizo moja lilopo Zanzibar ni kuwa chama ni kuto kutafauticha kazi za Serekali na kazi za Chama, hivi sasa tuna Serekali ya umoja wa Kitaifa SUK kuna wasio ccm wala cuf lakini ni Wazanzibar?.

    Sasa tutambue kuwa hakuna ulozima mtu kuwa mwanachama lakini kuna ulazima mtu kuwa Mzanzibar ikiwa ni mzanzibar.

    Sasa ikiwa mizizi yote ya ccm iko Dodoma na hata Rais wa Zanzibar hutolewa huko huko basi hii ni hatari kupangiwa mambo yetu kichama.

    ReplyDelete
  2. Ya Rabi wafunue akili viongozi wetu ili wawe na uchungu na nchi yao (Ameen),Mana Zanzibar tutachukua muda kuendelea kwa sababu Serekali yetu inaendeshwa kisiasa bila kuwa kujali maslahi ya Nchi.......
    Na hao wanaotufanya tuwe hivyo ( i.e baadhi ya Watanganyika kwa sababu sio wote wanafurahia dhulma tunayoipata wanzanzibar), wao wanabadilika na wanaijenga nchi yao kwa nguvu ila kwetu(Zanzibar) umasikini unaengezeka,
    Natoa mfano mdugu wenzetu walivyobadilika, Wao nafasi za ajira siku hizi zinatangazwa ili watu waombe na mwisho hupatikana mwenye sifa ila kwetu mpaka leo uwe umetoka maskani(na hao wamaskani mpaka wahonge) au uwe na jamaa......Wazee tubadilikeniiiiiiiiiii

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.