Habari za Punde

Zeco lapata hasara Pemba Milioni 1.6

Na Maryam Salim, Pemba
SHIRIKA la Umeme Kisiwani Pemba, limepata hasara ya zaidi ya Tshs, 1.6 milion, kutokana na watu wasiojulikana kukata miundo mbinu ya Umeme kwa kukata Waya wa Shaba mita mia nne (400).
Akizungumza na mwandishi wa Habari hiz, Meneja Wa Shirika hilo Tawi la Pemba, Salum Massoud, alisema kuwa Waya huo umekatwa huko Tungamaa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba , line ambayo inatumiwa na Wananchi kuanzia Michakaeni Chake Chake hadi Wete, jambo ambalo lilisababisha kukatika kwa umeme hafla.
Alielezea kuwa tukio hilo lililosababishwa na watu wasiojuilikana lilitokea majira ya saa 3.30 usiku , ambapo walitumia jiti na kifaa cha kukatia Waya ambacho kimeunganishwa na Jiti hilo.

Salum, aliwaomba Wananchi kulisaidia Shirika lao kwa kutowa taarifa pale ambapo wataona watu ama kikundi cha watu ambao wanaraslimali hiyo ama wanafanya hujuma hizo , kwani husababisha hasara kubwa watumiaji wa huduma hiyo.
Alifahamisha kuwa tukio kama hilo lilitokea usikuwa kuamkia Jumaatano, kwa kukatwa Waya kiasi cha mita 100 katika maeneo ya Meli tano, majira ya usiku , ambapo asubuhi yake vilionekana vipande vya waya huo .
Meneja huyo, alieleza kuwa pamoja na kwamba watu hao wameitia hasara Serikali lakini zaidi ni kwa Wananchi kwani wamepata hasara ya kukosa huduma muhimu kama vile Maji , umeme kwa ajili ya matumizi yao ya Nyumbani hasa wale wanaoishi katika mji wa Wete.
Hata hivyo meneja huyo, alisema kuwa tukio kama hilo sio la kawaida kutokea ingawaje kwa wiki hii matokeo mawili ya kukatwa kwa Waya huo limetokezea na kuitia hasara kubwa kuliko matukio yote yaliyotokea ndani ya Shirika hilo.

1 comment:

  1. Wakipatikana waliofanya hujuma hii wanyongwe!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.