Habari za Punde

Taasisi za kidini zatoa maoni kuhusu katiba mpya

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Mary Kashonda na Dkt. Sengondo Mvungi wakifuatilia mkutano kati ya Tume na Jumuiya ya Kidini ya Khoja Shia Ithnaasher Jamaats uliolenga kupata maoni ya taasisi hiyo kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo
Mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Kidini ya Khoja Shia Ithnaasher Jamaats Bw. Mohamed Dhirani akitoa maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo
Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Kanda ya Mashariki Mchungaji Mark Malekana (kushoto) akitoa maoni ya kanisa lake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam leo
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani akizunguma na viongozi Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) (kushoto) katika mkutano uliolenga kupata maoni ya kanisa hilo kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam leo
Sheikh Ibrahim Ghulaam wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini akitoa maoni ya Baraza hilo kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa wa Karimjee Jijini Dar es Salaam leo
 
Picha na tume ya katiba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.