Habari za Punde

Takwimu zitumike kuharakisha maendeleo

Na Kauthar Abdalla
KATIBU Mtendaji Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Amina Khamis Shaaban amesema upatikanaji takwimu sahihi ni muhimu kwa mipango kazi ya serikali na maendeleo kwa jumla.

Alisema katika juhudi za kukuza na kupunguza umasikini kwa maendeleo ya nchi suala utafiti una umuhimu mkubwa kwa kuwa ndio utakaosaidia kupatikana takwimu sahihi.

Alisema takwimu hizo zitasaidia watendaji katika ngazi mbali mbali kufanya maamuzi yenye ushahidi juu ya mipango bora kwa maendeleo ya watendakazi.

Alieleza hayo alipokuwa akifungua warsha ya uhamasishaji wa zoezi la utekelezaji utafiti wa hali ya utumishi nchini iliyofanyika ukumbi wa hoteli ya Bwawani.

Alisema hatua hiyo ni juhudi za serikali kuhakikisha mipango mikuu ya nchi inatekelezwa kivitendo ikiwa ni pamoja na dira ya manedeleo ya Zanzibar 2020 na MKUZA II.

Aidha alisema kuna ukaribu mkubwa baina ya mipango bora ya rasilimali watu na juhudi za kukuza uchumi na kupunguza umasikini katika maendeleo ya nchi.

Alifahamisha kuwa kufanya kazi kwa mipango mizuri ndiko kutakopelekea kupanua wigo wa soko la ajira pamoja na mipango bora kwa wale waliomo kazini.

Hata hivyo alisema juhudi zaidi bado zinahitaji kuchukuliwa na wadau mbali mbali kuhimiza mipango bora ikiwa ni pamoja na kuweka mazingatio juu ya matumizi ya za uzazi wa mpango.

Alisema matarajio ya serikali katika utafiti huo ni kuelewa uhalisia juu ya mahitaji ya wataalamu wa ndani ili iweze kupanga miakati itakayosaidia kupunguza changamoto zilizopo pamoja na kuelewa nafasi za kazi zilizo wazi katika soko la ajira.

Nae Kamishna Idara ya Kuratibu Shughuli za Idadi ya Watu ofisi ya Rais,Fedha,Uchumi na Mipango ya Manedeleo, Seif Shaaban Mwinyi akiwasilisha mada alisema madhumuni ya utafiti huo ni kutathmini uwezo wa taasisi za elimu na mafunzo katika upatikanaji wa taaluma inayohitajika katika soko la ajira.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.