Habari za Punde

CUF yawataka Wazanzibari kushikamana kuitetea Zanzibar

 Mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi la Chama cha C.U.F Juma Duni Haji akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Wanacha wa C.U.F katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Komba wapya Mjini Unguja.
 Baadhi ya Wanacha wa C.U.F wakicheza rusha roho kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Komba wapya Mjini Unguja
Baadhi ya Wanacha wa Chama cha wananchi C.U.F wakimsikiliza Mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi la Chama hicho Juma Duni Haji katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Komba wapya Mjini Unguja

Picha na Makame Mshenga, Maelezo

NA Maelezo Zanzíbar 02/02/2013
Mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi CUF Juma Duni Haji amewataka Wazanzibari kuongeza mshikamano na kujiepusha na itikadi za vyama vyao katika kutetea maslahi ya Zanzíbar kwenye Muungano.
Juma Duni ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wafuasi wa CUF katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kiwanja cha Komba wapya Mjini Zanzíbar.

Amesema njia pekee ambayo itawasaidia kupata maslahi wanayoyataka katika Muungano ni kuwepo kwa umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari jambo ambalo ni chachu ya mafanikio.
Ameongeza kuwa kwa muda mrefu Zanzíbar imekuwa ikibanwa na mambo mengi yanayohusu uchumi wake katika Muungano na kwamba sasa ni muda muafaka wa kupigania Muungano ambao utakuwa wa haki na usawa baina ya Zanzíbar na Tanganyika.
Juma Duni ambaye pia ni Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar amewataka Wazanzibari kuendeleza kudumisha amani iliyopo Zanzíbar sambamba na kutii sheria zilizopo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza Kuu CUF Ismail Jusa Ladu amedai kuwa Wazanzibari wanachotaka katika Katiba mpya ni Muungano ambao utatoa haki sawa baina ya Zanzíbar na Tanganyika.
Amedai kuwa Mshikamano ambao waliuonesha Wazanzibari katika kutoa maoni umewajengea uwezo watu wengine kutoka Bara kuwaunga mkono katika kutetea Muungano ambao unaipa hadhi Zanzíbar.
Mkutano huo umekuja ikiwa ni mwendelezo wa kuhamasisha uhai wa Chama na kutoa elimu ya Muungano kwa wanachama wa chama hicho.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBARI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.