NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu
Zanzibar Issa Haji Gavu, akimsikiliza Mfanyakazi wa Shirika la Bandari
Ramadhani Nomani wa sehemu ya Mnara wa Kuongozea Meli Zanzibar akitowa maelezo
jinsi ya kupokea na kuongeza meli zinapoingia Zanzibar, wakati wa ziara yake
kutembelea Signal Tower iliyohamishiwa jumba la ZSTC Kinazini
Naibu Waziri wa Mawasilianona Miundombinu Zanzibar Issa Haji Gavu, akimsikiliza mfanyakazi wa kituo cha Signal Tower, akitowa maelezo ya chombo cha AIS CM jinsi kinavyofanya kazi kutambuwa vyombo vilivyoko baharini kupitia chombo hicho, ambacho kimefungwa hivi karibuni kinauwezo wa kutambua mwenendo wa meli nakama kuna ajali imetokea katika eneo la bahari ya Zanzibar.
Kepteni Makame Haji akitowa maelezokwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Issa Haji Gavu, alipokuwa na ziara kutembelea kituo cha signal tower, katika jengo la ZSTC Kinazini
Mfanyakazi wa Signal Tower Ramadhani Nomani akitowa maelezo ya matumizi ya Chombo maalum cha Mawasiliano kinachotambua meli iliyoko bahaini na iko katika mwendo gani kinachojulikana kwa jina la AIS.CM.ambacho huwasiliana na Manahodha wa meli na kupata habari kama kutawa na ajali ya kuzama meli na majanga mengine ya baharini.
Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ya Redio kuongozea Meli na Vyombo vya Baharini Zanzibar Haji Juma, akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Issa Haji Gavu, alipofanya ziara kutembelea Signal Tower inaofanya kazi zake katika jengo la ZSTC Kinazini, baada ya jengo kuhama katika jengo la Belti Laajabu Forodhani kutokana na kubomoka katika sehemu ya jengo hilo.
No comments:
Post a Comment