Habari za Punde

Dk.Ndalichako atoboa siri ya wanafunzi kufeli

Na Mwandishi wetu
 
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako amesema kutowajibika kwa walimu, wazazi na wanafunzi ndio chanzo cha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani ya kidato cha nne.
 
Dk. Ndalichako alisema wanafunzi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kujihusisha na vitendo vya starehe, ikiwemo kujirusha katika kumbi mbali mbali za burudani. “Unapokwenda night club (kumbi za starehe) unakutana na wanafunzi wengi wanaofuata starehe badala ya kushughulikia masomo,”alisema wakati akizungumza na TBC.


Aidha alisema utandawazi umetumiwa vibaya na baadhi ya wanafunzi, ambao wanatumia mitandao ya kijamii kama tweeter na facebook kuchati na marafiki zao.
 
Kuhusu wazazi alisema wameshindwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao huku baadhi ya wanafunzi wakilazimika kujitegemea kutokana na wazazi kushindwa kuwajibika.
 
Wadau mbali mbali wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu matokeo hayo huku wengine wakisema walimu wamekuwa wakipuuzwa kwa muda mrefu hali inayowafanya wengine kuamua kuacha kazi kutafuta maslahi katika kada nyengine.
 
Akitangaza matokeo hayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Shukuru Kawambwa alisema asilimia 60 ya watahiniwa wamepata alama sifuri

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.