Na Mwandishi wetu
MAJAJI wa tunzo ya umahiri wa uandishi wa habari Tanzania (EJAT) wataapishwa leo katika hafla itakayofanyika ofisi za Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Majaji hao wataapishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya MCT, Jaji Mstaafu wa mahakama kuu, Thomas Mihayo.
Majaji hao ni Wenceslaus Mushi, Attilio Tagalile, Edda Sanga, Bernardina Chahali, Ngalimecha Ngahyoma, Yussuf Omar Chunda, Pili Mtambalike, Pedenciana Temba, Mwanzo Millinga na Anaclet Rwegayura.
Baada ya kuapishwa jopo hilo litaanza kujadili kanuni na mwongozo wa majaji na baadae kikao hicho kitahirishwa hadi Februari 25 wakati jopo litakapoanza kazi rasmi ya kupitia kazi zinazoshindaniwa.
Hii itakuwa ni mara ya nne kwa tunzo hiyo kuandaliwa.
No comments:
Post a Comment