Habari za Punde

Mbunge adaiwa kumpora mtu mke

 
Mbunge wa Ziwani, kisiwani Pemba, Ahmed Juma Ngwali
Mbunge wa Ziwani, kisiwani Pemba, Ahmed Juma Ngwali (CUF), amefunguliwa jalada katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, akituhumiwa kuvunja ndoa ya mfanyabiashara wa mjini Unguja na kutorosha watoto wawili nchini kwenda Canada, kinyume cha sheria.
Ngwali anatuhumiwa na mfanyabiashara huyo, Khalfan Said Chondoma, mkazi wa Saateni, kisiwani Unguja, kuingilia ndoa yake na kusababisha kuvunjika na hivyo kupata mwanya wa ‘kumpora’ mkewe.
Pia anatuhumiwa kutorosha watoto wa mfanyabiashara huyo msichana (8) na mvulana (9) na kuwapeleka Canada baada ya kuwabadili ubini halali wa baba yao mzazi na kuwapachika ubini wa mbunge huyo.
Khalfan aliliambia gazeti hili jijini Dar es Salaam jana kuwa aliripoti suala hilo katika kituo cha polisi Oysterbay na kufungua jalada namba OB/RB/21545/2012.
Khalfan (31), analalamikia kutoroshwa kwa watoto wake chini ya himaya ya wazazi na kuwa kabla ya matukio hayo, Ngwali alikuwa rafiki yake aliyekuwa akimtembelea nyumbani, lakini hakujua kuwa alikuwa ana lake moyoni dhidi ya mkewe.
Alidai kuwa alikuja kubaini hilo baada ya kuanza kuona uhusiano mzuri uliokuwa kati yake na mkewe awali ukibadilika ghafla.
Khalfan alidai uhusiano kati yake na mkewe uliendelea kuwa mbaya hadi ulipotokea mtafaruku mkubwa kati yao.
Alidai kufuatia mtafaruku huo, mkewe aliondoka nyumbani bila kupewa talaka na kwenda nyumbani kwa wazazi wake mkoani Tanga.
Khalfan alidai wazazi wake waliingilia kati mgogoro huo, lakini yeye akashikilia msimamo wake kwamba, ili ampokee na kuendelea kuishi naye sharti akubali kutofanya kazi kwa kuwa hana uwezo huo kutokana na elimu yake kuwa ya darasa la tano.
Alidai mkewe aliendelea kupinga sharti hilo na hivyo kukataa kurejea kwake.
Kwa mujibu wa Khalfan, wiki chache baadaye alisikia kuwa mkewe ameolewa na mbunge huyo bila kumpa talaka.
Alidai kuwa watoto wake walitoroshwa kwenda Canada, Oktoba 30, mwaka jana, baada ya mbunge huyo kuwapachika ubini wake.
“Aliwabadilisha ubini wao halali na kuwaita (anataja majina yao),” alidai Khalfan. Alidai hadi sasa watoto wake bado wanaishi Canada, ambako wao na mama yao wamejitambulisha kama wakimbizi. “Sijui wamejilipua kama wakimbizi wa nchi gani, maana Tanzania hatuna wakimbizi,” alidai Khalfan.
Hata hivyo, alidai kuwa taarifa alizonazo ni kuwa watoto wake walitakiwa kurudi nchini Novemba 7, mwaka jana, lakini haijulikani kwanini hadi sasa hawajarudi.
Alidai kufuatia kitendo hicho, aliwasiliana na Mtandao wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini, ambao aliwakabidhi vielelezo vyote vinavyohusiana na shauri hilo. Khalfan alidai Interpol walikwenda Zanzibar, pamoja na mambo mengine, walichukua vivuli vya pasi za kusafiria zilizoandikwa ubini bandia wa watoto hao.
Alidai baada ya kuchukua vielelezo hivyo, Interpol walimhakikishia kuwa wanaendelea kufuatilia suala hilo.
Khalfan alidai anachokitaka ni kujua Ngwali ana haki gani kisheria kukaa na watoto wake, pia serikali ifahamu kile alichokiita “udhalimu” aliodai kufanywa na mbunge huyo na vilevile anataka apewe watoto wake.
Khalfan alionyesha vielelezo mbalimbali, kikiwamo cheti cha ndoa kuthibitisha kuwa alifunga ndoa na Aisha Machi 11, 2004; pia vyeti vya watoto hao vya kuzaliwa kuthibitisha kuwa ni watoto aliowazaa na mwanamke huyo.

KAULI YA MBUNGE NGWALI
NIPASHE jana iliwasiliana na Ngwali kwa njia ya simu, ambaye alithibitisha watoto hao pamoja na mama yao mzazi, Aisha kuwapo Canada.
Ngwali alisema Aisha ni mkewe halali wa ndoa, lakini watoto hao ni wa Khalfan.
Alidai hakumbuki tarehe na mwezi aliofunga ndoa na Aisha, lakini anachokumbuka ndoa yao ilifungwa miaka miwili iliyopita baada ya mwanamke huyo kumkataa Khalfan kutokana na kumzuia kufanya kazi ya duka.
Ngwali alidai ndoa kati yake na Aisha ilifungwa wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, kwa idhini ya wazazi wa mwanamke huyo.
Ngwali alidai cheti cha ndoa kinachothibitisha kuwa alifunga ndoa na Aisha kipo, lakini kwa kuwa yeye husafiri mara kwa mara, hawezi kutembea nacho mkononi.
Alidai hakuwahi kuishi na watoto hao, bali walikuwa wakiishi na bibi yao mzaa mama Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.
Hata hivyo, alidai kuwa hakuishi muda mrefu na Aisha, kwani mwaka jana mwanamke huyo alifanya hadaa na kuondoka kwenye himaya yake na kwenda kuishi na watoto hao Canada, kinyume cha taratibu.
Alidai kuwa kufuatia kitendo hicho, aliuandikia barua Ubalozi wa Canada, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Jeshi la Polisi kuwaelezea kilichotokea kuhusiana na mwanamke huyo.
“Nilimwamini kama mke wangu, lakini akafanya kinyume,” alidai Ngwali.
Alidai awali, walipanga na Aisha kwenda Canada, akampa jukumu la kutafuta viza, lakini akiwa bungeni, mwanamke huyo aliamua kuondoka kinyemela kwenda nchini humo.
Ngwali alisema anamshangaa Khalfan kumsikia akimtuhumu kutorosha watoto wake na kudai yeye hana shida ya watoto wa mtu mwingine, kwani tayari anao watoto wanne aliozaa na mkewe wa kwanza.
“Huyu bwana anacholilia ni wivu tu wa mapenzi. Haya mambo ukiyasikia ni ya ajabu. Kwani aliwahi kunitaka nimfidie. Hao watoto siyo wangu, vipi unilalamikie mimi?” alihoji na kuongeza: “Anataka kunichafulia jina.”
Alimshauri Khalfan kwenda mahakamani, akidai huko ndiko haki inakotolewa badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari ili kumchafulia jina, kwani kwa kufanya hivyo hakuna faida yoyote anayoweza kuipata. Alidai pia anamshangaa Khalfan kumtuhumu kwamba, amebadili majina ya watoto wake bila kuthibitisha tuhuma hizo.
Ngwali alidai kwamba ni jambo lisilowezekana kubadili majina ya watoto kwani ilitakiwa aende kufanya hivyo mahakamani.
Pia alidai tangu azaliwe hajawahi kwenda mkoani Tanga na watoto hao hawamo kwenye pasi yake ya kusafiria.
“Mimi hawa watoto siyo wangu. Ninao wangu wa halali. Kama kuna mtu kabadilisha majina yao, mimi sijui. Na atoke mtu yoyote duniani athibitishe hilo, nitawajibika,” alidai Ngwali na kuendelea:
“Yule mwanamke ana asili ya Kiarabu na Khalfan ana asili ya Kiarabu. Mimi ni Mswahili. Hiyo ndiyo asili ya chuki na huyu bwana. Kwamba, kwanini Mswahili aoe Mwarabu? Sasa tatizo hapa siyo watoto, bali tumkomoe.”
Ngwali alidai kama ni uchungu, basi yeye ndiye anayeumia zaidi kwani alikuwa akiwalipia watoto hao ada ya shule Shilingi milioni tatu kwa mwaka.
“Hivyo, yote anayosema ni uwongo. Anataka aonewe huruma. Ni wivu tu wa mapenzi ndiyo unaomsumbua. Kwa hiyo, hiyo story (habari). Ni watu wanaogombea mwanamke na sote tumemkosa.”
Ngwali alidai sehemu kubwa ya maelezo hayo aliyatoa alipohojiwa na vyombo vya dola, ikiwamo interpol.

KAULI YA POLISI
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kinondoni, John Mtalimbo, alisema taarifa za Khalfan kufungua jalada hilo katika kituo hicho alizisikia jana, hivyo alimtaka mwananchi huyo kwenda ofisini kwake leo asubuhi ili kujua suala lake lilipofikia.
Hata hivyo, alisema kwa jinsi lilivyo, suala hilo ni kubwa, ambalo hata kama jalada lake lilifunguliwa katika kituo hicho, bado linahusiana na Interpol. Pia NIPASHE ilijaribu kuwasiliana na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, kueleza sababu za shauri hilo kuchukua muda mrefu, lakini hakupatikana.
Alipopigiwa simu yake ya mkononi ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake, ambaye alisema angemfikishia bosi wake ujumbe wa kutafutwa na mwandishi.
 
CHANZO: NIPASHE

10 comments:

  1. Kitu kimoja hakiko clear. Jee huyu mwanamke aliachwa na Khalfan kabla ya kuolewa na huyu mbunge? Kama hakuachwa ilikuwaje huyu mbunge akaoa mke wa mtu kwasababu ndoa haiwezi kusihi kama mwanamke hajaachwa. Haya mambo ya wivu na uarabu ni kujaribu kupotosha issue yenyewe.

    ReplyDelete
  2. khalfan chondoma wacha mambo y kitoto ww sio wamwazo kukimbiwa na msichana
    kupakaziana kwenye mitandao huyo alikuwa mama watoto wako nenda katafute binti mwengine uowe ok bulabula sio mzuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Khalfan alimuacha huyu mwanamke na hakuchukua muda alioa mke mwengine. Lakini huyu mbunge ni kweli alikuwa akipiga ndogondogo kwa mke wa Khalfan kabla ya kuachika. Unajua Huyu mbunge alikuwa ni jirani na huyu mwanamke alieolewa na Chondoma tokea walipokuwa wadogo pale Machomane. Sasa nadhani haya ni mambo aliyoyaimba Abdalla Issa ya "pendo ni pendo la kwanza..... wazamani ukimuona...".
      Haya mchezo nauendelee.

      Delete
  3. Halfani usiongee uongo ukweli ulimuacha aisha na alikaa mwaka mzima ndio akaolewa na mbunge kisha ulikuwa huwasaidii wanao hata shilingi unataka kupakaza ubaya huna lolote we elimu huna labda ukawadanganye wajinga km wewe, mshukuru mbunge kukusaidia kustiri wanao wewe acha kuongea pumba

    ReplyDelete
  4. Una roho mbaya tu ulipomuacha aisha ulijua ataadhirika huna lolote roho mbaya inakusumbua.usiokaa ukaomba mungu wanao wafanikiwe waje kukufaa baadae we unapigania uwarudishe pumbavu kabisa elimu finyu unaonekana hakuna mtoto atakaemsahau mzee wake wewe tafuta shule ukasome ushafulia

    ReplyDelete
  5. Na uache bangi unazovuta wewe bogas unajidhalilisha shenZi zako kabisa na bado ulivyochanganyikiwa mpk utavua nguo barabarani kwa bangi unajitapa unapesa mbona unalia unasema umeliwa pesa na hao interpool wako umeuza mpk kipikipiki chako shenzi kabisa huna akili wewe unawaza ujinga tu watu wanapigania pesa we unapigania upumbavu

    ReplyDelete
  6. Eti unasema aisha hakwenda shule ulipomuacha mbunge kampeleka shule hongera mbunge, huyu bogas anamuacha mtoto mzuri ulijua atachina wenzzio wameokota dhahabu kkoo wafanyaje ondoa upumbavu wewe mpemba fyoko tu wewe

    ReplyDelete
  7. Naona siri zinafichuka tu tuliza boli achana na roho mbaya. mmh kumbe ulimuacha ah nilimuona pale saateni na ningejuwa kama ndo ushamuacha basi ningemtafuta katoto kazuri cha kuweka ndani kile. pole sana

    ReplyDelete
  8. maneno ya mkosaji hayoo,we khalfani chakubimbi tuu si ulimuacha ukaoa kwa vifijo na nderemoo ushafuliaa na kuanika,mpfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. na karibu utakua chizi wewe


    ReplyDelete
  9. pumbavu wewe hilooooooooooooooooooooooooooo endelea tuu kama umeliwa pesa sasa hivi zamu yako hao interpol wako watakula kiboga, akili zako zimejazwa lima,

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.