Habari za Punde

Kuuwawa kwa Padri Mushi

          Padri Evaristitus Mushi                
         TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                                                                                
Padri Evaristitus Mushi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya ST.Joseph,Shangani,Unguja ameuwawa leo mnamo saa moja asubuhi katika eneo la Beit-EL-Ras karibu na kanisa la Katoliki.la Betras

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Waziri wa nchi  Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud imeeleza kuwa kutokana na tukeo hilo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatambua wale wote waliohuka na tukio hilo kwa ajili ya kuwachukulia hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria.

Aboud amesema kuwa wakati uchunguzi huo unaendelra, Serikali inawaomba wananachi wote kuwa watulivu na kuliachia Jeshi hilo la Polisi kutekeleza wajibu wake .

Aidha Serikali imetoa mkono wa pole kwa familia na wanafamilia wa marehemu pamoja na waumini wa kanisa hilo kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
178/2/2013

5 comments:

  1. Hapa nafikiri kuna mchezo unachezwa.. maana mambo haya hayakuwepo zamani hapa Zanzibar..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana na wewe.Wanaofanya vitendo hivi inaonekana sio wazanzibari. Hawa ni watu wanaokuja kutoka bara kwa ajili ya kuhujumu maelewano kati ya Waislamu na Wakristo ili Zanzibar ionekane kama ni nchi ya kigaidi muda ukifika tukaanza kudai nchi yetu.
      Inasikitisha sana.

      Delete
  2. Maoni ya wadau hapo juu ni muendelezo wa mawazo yetu 'mgando' wa zanzibari kwamba eti sisi ni watakatifu sana na hatuwezi kufanya maovu.

    Ndugu zangu tusijidanganye, ubaya hauna kwao! na mfano mzuri ni matukio mbali mbali ya ujambazi yaliyowahi kutokea Z'bar, ambayo yalihusika pia wazanzibari.

    Aidha, tuna mifano ya vijana wetu wanaotumikia vifungo Mrekani kutokana na vitendo vya ugaidi.

    Ni kweli kwamba Z'bar haturuhusiwi kumiliki silaha lkn. hii haiondowi uwezekano wa vijana wetu kuziingiza kinyemela kutoka Bara na kufanya uhalifu.

    Kwa kweli tunahitaji ku'exercise ojectivity' wakati tunaangalia suala hili na sio ku'jump into conclusion'

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lakini wanaoweza kuingiza silaha kutoka bara nadhani ni wazanzibara. Lakini pia kuingiza silaha kitu kimoja lakini uwezo wa kuitumia kwa staili za hawa waliompiga risasi padri unashangaza. Unajua hawa jamaa wana ujuzi wa hali ya juu kama ule wa kijeshi. Pia wanaweza kufanya uhalifu kisha wakapotea bila ya kujulikana. Kama ni watu wa Zanzibar basi ni watu vikosi vya serikali kwasababu wao ndio wanaoweza kutumia silaha. Mafunzo ya silaha kwa wazanzibari wa kawaida hayajulikani. Wazanzibari waliokamatwa kwa ujambazi, wamekamatwa kwa kutoa ushirikiano wa uhalifi ambao wanajua ukifanikiwa watapata pesa. Uhalif huu unaeleweka. Lakini uhalifu huu wa kutaka kuleta fitna katika jamii kwa kuua au kudhuru viongozi wa dini, hapa unatusingizia wazanzibari.Hakujawa na network za uhalifu kama huu.

      Delete
  3. Kimsingi sina nia ya kuwanyooshea vidole W'bari kwa kuhusika na tukio hili, lkn. tikurupuke na kudai eti vijana wetu hawawezi.

    Kumbukeni AHMED KHALFANI GHAILANI aliyefungwa marekani kwa sasa, alikamatwa Pakistani baada ya majibizano ya risasi na FBI kwa masaa sita! na yule kijana wa hapo bububu na malindi!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.