Wadau wangu natowa Tahadhari na Wizi ulioingia sasa katika katika Visiwa vya Zanzibar kupitia njia ya simu kujitambulisha kuwa yeye ni mzazi wako au ni ndugu wa karibu na wewe na kutaka kumsaidia pesa kutatua matatizo yake.
Mkasa huu ulitaka kunikumba jana wakati nikirudi kazini mara nikapigiwa simu na mtu akijifanya ni mama yangu kunitaka nimtumie Pesa kupitia Tigo Pesa ana matatito kupitia Namba hizi na m 0777151720 na 0717727563.
Kwa hiyo nawatahadharisha Wadau na wizi wa aina hii kupitia mitandao ya Simu kutaka kuwaibia Wananchi kwa njia hii.
Asante kaka , na pole ingawa hukuingia mtegoni. Vyombo vya ulinzi viko wapi ? Je ule usajili wa namba si ulikuwa utumike kuwasaka hawa ? Ukiwauliza tume ya mawasiliano watakuletea stori ndefu ziso maana
ReplyDelete