Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emanuel Nchimbi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Kilimani kutokana hali ya tukiolillilotokea leo asubuhi la kuuwawa Padri wa Kanisa la Betras wakati akiende kuongoza Sala ya asubuhi kanisani hapo na kushambuliwa na watu wasiojulikano kwa risasi na kufariki dunia.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emanuel Nchimbi, kutowa taarifa ya Serekali kuhusiana na tukio hili la kushambuliwa kwa silaha Padri Everest Mushi wa Kanisa la Betras Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emanuel Nchimbi akitoka katika chumba cha mkutano baada ya kutoa Taarifa ya Serekali kuhusiana na tukio hilo mazungumzo hayo yamefanyika ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar.
Gari ambalo alikuwa akitumia Padri Everest Mushi likiwa katika ukuta lilipoingia baada ya kushambuliwa na Watu wasiojulikana na kuingia katika moja ya nyumba ilioko kando ya barabara ya bububu jirani na Kanisa hilo lilikotokea tukio hilo.
Hivi ndivyo ilivyokuwa baada ya tukio Wananchi wakiwa katika eneola tukio kuangalia na kuchukuwa picha za kumbukumbu ya tukio hilo, kama inavyoonekana picha ya juu na chini. 
Pandri Cosmas Shayo wakizungumza na Viongozi wa Kanisa kuhusiana na tukio hilo wakifanya taratibu za kisheria ili kukamilisha kuupata mwili wa marehemu.
Waumini wakiwa na majonzi ya Kifo cha Padri wao
Waumini wa Dini mbalimbali wakiwa katika viwanja vya Hospitali ya Mnazi Mmoja wakipashana habari na kupanga maandalizi ya Maziko wakiwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment