Viongozi wa NSSF na ZSSF wakiisalimia timu ya NSSF kabla ya mchezo kuaza na wenyeji wao timu ya ZSSF uliofanyika wanja wa Amaan.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman, akimkabidho kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Kirafiki wa Pasaka Nahodha wa timu ya ZSSF,baada ya kuishinda timu ya NSSF katika mchezo huokwa mabao 4--2.
Pashapasha ndivyo inavyoonekana wakisema wachezaji wa timu ya NSSF kabla ya kuaza kwa mchezo wao na wenyeji wao ZSSF, uliofanyika uwanja wa Amaan na kupata kipigo cha mabao 4---2
Wachezaji wa timu ya ZSSF wakisalimiana na Wageni wao wa timu ya NSSF kabla ya mchezo wa kirafiki kuaza kusherehekea michezo ya Pasaka
Beki wa Timu ya ZSSF akijiandaa kumpita mchezaji wa timu ya NSSF
Viongozi wa ZSSF na NSSF wakifuatilia mchezo wa kirafiki wa timu zao uliofanyika uwanja wa Amaan.
Mchezaji wa timu ya NSSF akimpita beki wa timu ya ZSSF katika mchezo wa kirafiki wa Pasaka uliofanyika katika uwanja wa Amaan.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakifuatilia mchezo wao wa kirafiki na wageni wao timu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Tanzania, uliofanyika katika uwanja wa Amaan, timu ya ZSSF imeshinda kwamabao 4---2
Mchezaji wa timu ya ZSSF Morris Amros akiifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo huo kwa shutu la mbali.
Mchezaji wa timu ya NSSF kushoto na mchezaji wa timu ya ZSSF wakiwania mpira katika mchezo wa kirafiki wa pasaka uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya ZSSF imeshinda kwa peneti 4--2
Wachezaji wa timu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wakimfariji mchezaji wa timu ya NSSF ambaye amekosa peneti katika mchezo huo na kufungwa na timu ya ZSSF kwa mikwaju ya peneti.
Wafanyakazi wa ZSSF wakiwa na furaha baada ya kutowa Kombe la Urafiki wa mchezo wa Pasaka na wageni wao NSSF, kwa kuwafunga 4-2.
Wachezaji wa Timu ya Mfuko wa Hifadhi ya Taifa Zanzibar ZSSF , wakiwa na Viongozi wao katika picha ya pamoja na kombe lao la Ubingwa wa michezo wa Kirafiki na timu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Tanzania NSSF, Baada ya kuifunga timu hiyo kwa mikwaju ya peneti. Timu hizo zimetoka sare ya 2--2 katika mchezo wa kwaida na kuamuliwa kupigwa kwa peneti na timu ya NSSF imepata peneti 2 na kukosa mbili nayo timu ya ZSSF imepata peneti 4 na kuwa bingwa kwa mwaka huu wa michezo ya Pasaka kwa mara hii imnafanyika Zanzibar na kutembelewa na wanamichezo wengi kutoka Tanzania Bara.
Mchezo huo wa kirafiki wa Pasaka umefanyika katika uwanja wa Amaan na mgeni rasmini katika mechi hiyo alikuwa Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika walimu Haroun Ali Suleiman, amekabidhi kombe kwa bingwa wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment