Habari za Punde

Usafi wa Mazingira Mitaani ...

Mfanyabiashara katika eneo jirani na duka la Suma Darajani akifanya usafi katika eneo lake la biashara kuweka mazingira safi kwa wateja wake, kutokana na moja ya karo katika eneo hilo kufurika maji machafu na kutoka nje kutapakaa katika eneo hilo, akiweka njia kwa ajili kupitishia maji hayo katika moja ya karo lilioko karibu na eneo hilo.
 
Kama anavyoonekana akiwa katika harakati hizo kuweka njia ya kupitishia maji hayo. Makaro haya hufurika maji kutokana na kuziba kutokana na matumizi mabaya ya Wananchi wakiwa katika majumba yao kuweka matambara na vitu vya kuoshea vyombo husababisha hali hii na kuwa usumbufu kwa watumiaji wa njia hiyo kwa kutapakaa kwa maji machafu katika maeneo hayo baada ya kuziba na maji yake kusambaa njiani

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.