Habari za Punde

Bunge laanza leo Mjini Dodoma.

Na Mwandishi wetu
MKUTANO wa 11 wa Bunge la bajeti ya Serikali ya Tanzania unaanza leo katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.

Mkutano unafanyika huku wananchi wakiwa na kumbukumbu ya matukio ya kurushiana maneno na kile kilichoelezwa na Spika Anna Makinda, utovu wa nidhamu katika kikao kilichopita cha mwezi Februari.

Mkutano huo ulisababisha bunge kusitisha kupokea hoja mbali mbali binafsi zilizowasilishwa na wabunge huku ikiundwa tume kuchunguza ghasia hizo.

Kikao cha bajeti kwa kawaida hufanyika mwezi Juni, lakini mwaka huu kimelazimika kufanywa mapema ili kutoa nafasi kwa wabunge kushiriki katika bunge la katiba.

Wananchi wanatarajia mkutano huo utafanyika kwa ustaarabu wa hali ya juu, huku wengine wakiwa na hofu ya kuendelea kuwepo msuguano.

Tayari wabunge wameshawasili katika viwanja vya bunge huku wengine wakiwa njiani kuelekea Dodoma.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.