Habari za Punde

Nahodha awatolea uvivu mafisadi Zanzibar

Na Mwinyi Sadallah
 
Waziri Kiongozi mstaafu wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha, amesema hoja ya kuwapo au kutokuwapo kwa hati ya Muungano kusifute azma ya kuwashughulikia viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali za umma Zanzibar .
Nahodha aliyasema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mzalendo Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani hapa.
Alisema ameshangazwa na baadhi ya viongozi wakitunisha misuli kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati baadhi yao wakikabiliwa na tuhuma za unadhirifu ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
Alisema Zanzibar inakabiliwa na matatizo makubwa ya matumizi mabaya ya ardhi kwani viongozi wengi walijimegea kwa maslahi binafsi na wanajulikana.
Akifafanua zaidi alikiri kuwa kero za Muungano zipo na zinaeleweka ingawa alisema baadhi ya watu wakiwamo viongozi wanatumia mwanya huo ili kuficha tuhuma za ufisadi, uporaji na kujipatia utajiri usioelezeka.
"Kuhoji kuwapo au kutokuwepo kwa hati ya muungano baada ya miaka 49 kupita ni sawa na mtu kupatwa shaka kuhusu uhalali wa cheti cha ndoa ya wazazi wake, je ikiwa kimepotea kinaweza kubatilisha ndoa na uhalali wa mtoto,?"alihoji Nahodha
Alisema wanaotaka Muungano wa mkataba nia na lengo lao ni kuvunja muungano uliopo ili wapate nafasi ya kuatamia utajiri waliopata kwa kupora mali za wananchi na serikali yakiwamo majengo ya umma kinyume na sheria.
Aidha, aliwataka viongozi wa serikali na wanasiasa kujenga utashi na ujasiri wa kuhoji kwa nguvu ya hoja na kukemea vitendo vya ufujaji vilivyokithiri na kusababisha uchumi wa Zanzibar kutoimarika.
Alisema bado kuna vitendo hatarishi katika taasisi za serikali hivyo ni jukumu la kila mwenye ujasiri akapaza sauti yake badala ya kutumia muda mwingi kujificha kwenye kivuli cha hati ya Muungano.
Nahodha ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alisema Serikali ya CCM itaendelea kutetea msimamo wake wa muundo wa Serikali mbili na kushughulikia kasoro na utatuzi wa kero zilizopo katika Muungano bila kuyumbishwa na kundi lolote.
Akizungumzia upotevu wa Sh. bilion 20 katika Shirika la Umeme Zanzibar(zecco), alisema fedha hizo ni nyingi na zingeweza kutumika kusukuma maendeleo ya kisekta na badala yake akasema zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.
"Tusijifiche chini ya kivuli cha hati ya muungano wakati baadhi yetu mikono yetu inachuruzika michirizi ya uporaji, wizi na ubadhirifu wa mali za umma na uvunjaji wa sheria,"alisema Nahodha huku akishangiliwa.
Akilizungumzia suala la vijana kukosa ajira, alisema ni hatari kulisahau kundi hilo la vijana kwa kuwa ndiyo lenye nguvu na ushawishi.
"Chama chetu kihakikishe kinachemsha bongo na kulishika kundi hilo, lipewe nafasi katika medani za uongozi wa leo, kujengewa uwezo ili liwe jeshi imara litakalokabili mapambano na kuwashinda maadui,"alisema Nahodha .
Matamshi ya Nahodha yamekuja huku Serikali ikiwa bado haijatekeleza ripoti tatu za Baraza la Wawakilishi za kuchunguza matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu ikiwamo uuzaji wa ardhi kwa maslahi binafsi na majengo ya Serikali.
Ripoti ya kwanza ilihusu uuzaji wa majengo katika hifadhi ya mji wa urithi wa dunia katika mji mkongwe aa Zanzibar, kisiwa cha changuu kilichokodishwa kwa bei ya kutupa,ubadhirifu katika Zecco na Baraza la Manispaa Zanzibar.
Ingawa ripoti zote zimesema kuna viongozi na watendaji wanaotakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuuza mali za serikali kwa kutozingatia sheria ya manunuzi na ugavi lakini hadi sasa hakuna kigogo yeyeto aliyefikishwa mahakamani
 
Chanzo - Nipashe

8 comments:

  1. Unafiki tu kwani Tanganyika hakuna walioiba kuliko Zanzibar? Watanganyika wanatuibia Wazanzibari sote na hili ndilo la muhumu kwanza halafu yaje haya uliyoysame na sio hili tu na landege kupaki najani ya ng'ombe pia na mengi mengineo!!!!!

    ReplyDelete
  2. Shamsi umeongea zaidi kichuki kuliko uhalisia,ss tunajua umeondoka madarakani ukiwa na bif na mh karume lakini kumbuka kua kwa uwezo wa Allah na Amani leo usingekua hapo.Ss tunajua Amani karume kachukua vitu vingi lakini hatuwezi kuwa watumwa wa vibaraka wa tanganyika akina nyinyi kwa kutoacha kumsamehe Amani kwa jambo kubwa alilolifanya la kihistoria,unajua mtu anahukumiwa kwa khatima.Ww ulifanya mangapi tunayajua, Tanganyika kuna wizi wa kuua mbona huyasemi huko. La msingi hivi ss ni kupata Zanzibar iliyo huru

    ReplyDelete
  3. Maneno yote aliyoyasema Mh. Waziri ni kukasirika kwake kwa wale wanaotaka Zanzibar iwe na nchi yake na mamlaka yake.
    Tatizo letu ni viongozi wetu waliogawanyika wasio na msimamo mmoja kwa masilahi ya nchi kama huyu waziri, viongozi wetu wote ni woga na hawaoni mwelekeo wa Zanzibar wa siku za mbele na vizazi vijavyo. Huyu waziri ni wa aina hiyo ya viongozi wanaopendelea ukubwa na fahari ya binafsi. Mawazo yake yamepitwa na wakati na jambo la kusikitisha anafurahiya kuendelea kumezwa kwa visiwa hivi vya Zanzibar. Mh.Waziri unaposema viongozi waliojikushanyia mali na kuwatia umasikini Wazanzibari miaka 49 sasa ni wafisadi, mimi nahisi pia waziri ni mfisadi kwani anaelewa vizuri kwamba nchi hii inaongozwa na chama chake kwa muda wote huo wa miaka 49 na yeye aliwahi kuwa mmoja wa viongozi wakubwa hapa visiwani, mbona hakuchukuwa hatuwa yeyote. Huyu ni kati ya madikteta wetu , kwani anasifa hizo, ni mtu aliyezowea asante bwana. Fikira nyingine zozote zinazopingana na zake utakuwa aduwi.
    Mbona hakufafanua kwamba hata hiyo ndowa ya miaka 49 mtu anaweza akawachana na mke wake, na uhalali wa watoto katika karne hii zitatambulika kwa njia ya DNK, leo uhalali wa muungano huu uko wapi. Kuna nchi nyingi duniani zilizotengana baada ya miaka isiyopungua 60 na nyingine miaka 100 na zaidi. Tujisomeshe History kidogo jinsi nchi zilizokuwa pamoja na leo zimevunja muungano waliokuwa nao na jinsi wanavyonufaika. Hata mivutano ya kisiasa na kutoaminiana umetoweka na manufaa yametokea na hata ujirani na udugu umeimarishwa.

    ReplyDelete
  4. Alichokisema mh.Shamsi ni sahihi na hatua za haraka zinahitajika ili kuiokoa Z'bar na balaa kubwa la ufisadi linaloelekea kuifisidi nchi.

    Sasa hivi naanza kupata picha kwa nini ufisadi Z'bar hawishi kumbe ni sisi wenyewe tualea!

    Maoni ya wadau hapo ni ushahidi wa wazi wa kulea ufisadi, lazma tufikie hatua tuchukie ufisadi bila kujali ni nani aliyeusema!

    ReplyDelete
  5. Kama muheshimiwa anataka kuongea kuhusu ufisadi Zanzibar he needs to talk about Muungano kwanza huu ndio ufisadi mkubwa but to point finger to some people na kuweka picha kubwa ili aonekane kuwa anaitetea Zanzibar!!! This is wronge!! Kwa sababu naamini kuwa Mh hana nia hiyo Bali anajaribu kujipanga katika nafasi nzuri ya kutaka kugombea nafasi ya Uraisi. Hili ndio lengo lake! Talk about TRA, talk about miundo ya Wizara za Muungano, Talk about wanafuzi kufelishwa....Talk about Serikali kivuli ya Tangayika kwa jina la Serikali ya Muungano! Hii ni Serikali ya Tanganyika lakini Waiita Serikali ya Muungano!!! Mbona yapo mengi ya kuonge??? Kwa Faida ya Zanzibar !!!!! Just he needs to be open!! Ila hili analofanya yeye ndio ufisadi kwani halitojenga Wazanzibari bali litawagombanisha lakini akiongea moja tuu ya issue kama kufelishwa kwa wanafuzi hili liwajenga Wazanzibari kuwa kitu kimoja!!

    ReplyDelete
  6. Ndugu yangu muungano unazungumzwa sana labda useme hauzungumzwi kwa namna wanayoitaka UWAMSHO!

    lazma tukubali huu upo tu, madam sisi wenyewe tunashindwa kuzungumza kwa sauti moja na kuelewana.."let's get prepared for worse"!

    Mimi nadhani hii, sio bure itakua W'bari tulimkosea M/Mungu kitu akatulaani..haiwezekani kiongozi akemee uovu, aekewe masharti ya kukemea!

    Leo hii Muungano umekua ndio chaka la watu kufichia maovu yao..angalia mifano;

    Mashirika kama ZECO,ZSSF,ZRB Bandari na Airport watu wanapora fedha kama wana wazimu, ukiuliza, unaambiwa matatizo ya muungano!

    Tuje wizara ya ardhi, watu wanagawana mashamba na viwanja kule Tunguu kama Z'bar ni ya kwao peke yao, ukiliza..matatizo ya muungano!

    Idara ya vitambulisho nayo kwa kushirikiana na masheha inawanyima baadhi ya W'bari vitambulisho, akina nyinyi mnasema ni matatizo ya muungano!

    Wakati wa 'KOMANDOO' ndege(jet) ya SMZ ilipelekwa kubeba majani ya ndege ikapata hitilafu na kututia ufukara mpaka leo hatujamiliki tena ndege...eti nalo ni tatizo la muungano!

    Wizaratu..t'aalim nayo inashindwa kusimamia elimu vizuri huku wakipika matokeo ya form 2 ili ionekane watoto wamepasi wengi, hatimae wakifeli form4..tunaonewa..matatizo ya muungano!

    Angalia 'stone town' kivutio pekee kikubwa cha utalii Visiwani na urithi wa Dunia watu wanaruhusiwa kuongeza ghorofa na kuishia kuporomoka ukiuliza..matatizo ya muungano!

    Jamani, kwenda skuli ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo lakini kwa mitazamo hii tuliyonayo..mimi nadhani hatuna haja ya kwenda tukiwapa watu pesa bure vyuoni wakila!

    ReplyDelete
  7. Kwa watu sisi tulikuwa hatukenda skuli wala hatuna uwezo wa kufikiri!!' Just a simple question !!! how to fix this problems??? Kwenye majukwaa ya CCM na kuhubiri au? Tusaidieni mlokwenda skuli wenye uwezo wa kufikiri!!! Use your intellectual brain!!! Professional !!! The capacity of thinking you have to solve these problems!! Ili na sisi tufaidike with your intelligence!!!

    ReplyDelete
  8. Ndugu yangu mwenye uwezo wa kufikiri... Huyo Nahoda na hao wakuu wa Tasisi ulizozitaja wanatoka chama gani? Tunaomba mawazo yako. Wako hapo to implement sera za chama chao cha CCM!! So this is the Consequences! Au unamawazo gani ndugu yangu !!! Hili letu sote let's share the ideas.....

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.