Habari za Punde

Kikundi cha Mazoezi cha Mwenge Chatimiza Miaka Minne


 


 Kikundi cha Mazoezi kutoka Jambiani wakionesha jinsi ya umuhimu wa mazoezi kwa Mwanadamu.





 Vijana hawa wakionesha umahiri wa mazoezi kuwa ni afya kwa mwanadamu, wakipita mbele ya mgeni rasmin.
 Vikundi mbalimbali vya Mazoezi vikifanya mazoezi ya pamoja katika kusherehekea miaka minne ya kikundi cha mwenge.

 Mambo ya Kikundi cha Mwenge wakati wa kifanya mazoezi ya viungo katika sherehe yao ya kutimia miaka minne tangu kuazishwa kikundi hicho zilizofanyika katika viwanja vya mwenge.kwerekwe C.
 Wanachama wa Kikundi cha Mazoezi cha Mwenge wakionesha umahiri wa jinsi ya kufanya mazoezi ya viungo kwa kucheza na ringi la baskeli ikiwa ni shamrashamra za sherehe hiyo kuonesha jinsi ya mafanikio ya mazoezi kwa mwili wa binaadamu.
Mgeni Rasmin wa tamasha la kuadhimisha miaka minne ya Kikundi cha Mazoezi cha Mwenge Mhe. Haji Omar Kheri akiwahutubia wanamichezo wa Vikundi vya Mazoezi katika hafla ya kusherehekea miaka minne ya kikundi hicho iliofanyika katika viwanja vya Mwenge Kwerekwe C. na kuhudhuriwa na jumla ya Vikundi 27 vya Mazoezi Zanzibar.
Mgeni wa Rasmini katika maadhimisho hayo Mhe Haji Omar Kheri, akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Mwenge Dau Hamad Mchango wake kwa kikundi hicho amekabidhi shilingi laki nne.
Mwakilishi wa Kikundi cha Mazoezi cha Mwenge chenye makaazi yake Mwanakwerekwe Unguja akisoma risala ya Kikundi chao kwa mgeni wa Maadhimisho hayo ya kutimia miaka Mnne ya kikundi hicho yaliofanyika katika kiwanja cha cha Mwenye Kwerekwe C.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.