Habari za Punde

Misumeno ya moto kutokomezwa

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiichoma moto misumeno ya moto 23 katika eneo la Kizimbani Pemba, ikiwa ni kampeni ya kutokomeza misumeno hiyo Zanzibar.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akishuhudia misumeno ya moto 23 katika eneo la Kizimbani Pemba, ambayo imekusanywa kwa ajili ya kuchomwa moto, ikiwa ni kampeni ya kutokomeza misumeno hiyo Zanzibar
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo na Maliasili, Mtumwa Kheir Mbarak akizungumza katika hafla ya uchomaji moto wa misumeno ya moto 23 katika eneo la Kizimbani Pemba.
 Mtumiaji wa nishati mbadala itokanayo na kinyesi cha ng’ombe Hamad Juma Hassan, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na utengenezaji wa nishati hiyo, wakati Maalim Seif alipomtembelea nyumbani kwake Kinyasini Pemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affan Othman Maalim, akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kuhusiana na maendeleo ya kilimo cha mpunga wa majaribio kisiwani Pemba. (Picha, Salmin Said, OMKR).

Na Hassan Hamad , OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka wananchi kushirikiana kuisaka misumeno ya moto popote ilipo ili iweze kutokomezwa kabisa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
 
Ameeleza hayo katika kampeni maalum ya kutokomeza misumeno ya moto ambapo misumeno 23 imechomwa moto mbele ya kiongozi huyo, baada ya kukamatwa na maofisa wa Idara ya misitu.
 
Amesema kila mtu ana wajibu wa kushirikiana na jamii katika kufichua misumeno iliyobakia, ili kuhakikisha kuwa haitumiki tena na kusababisha athari za kimazingira.
 
“Kila mtu ana wajibu wa kuwafichua watumiaji wa misumeno hii, lakini mashena na polisi jamii muna jukumu kubwa zaidi, na nina hakika mukiamua munaweza kuwabaini wote wenye misumeno ya moto”, alisema Maalim Seif.


Amesema iwapo misumeno hiyo haitodhibitiwa inaweza kuiathiri nchi kwa kiasi kikubwa kutokana na uwezo wake wa kukata miti kwa muda mfupi.
 
Uchomaji huo wa misumeno ya moto 23 umefanyika katika ofisi za Idara ya misitu iliyoko Kizimbani Kisiwani Pemba.
 
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya kilimo na maliasili Affan Othman Maalim amesema misumeno ya moto ipatayo 270 bado inakisiwa kuwepo Zanzibar, na kwamba kampeni hiyo itasaidia kuitokomeza.
 
Kwa mujibu wa Affan, kisiwa cha Pemba kinaongoza kwa kuwa na misumeno mingi ya aina hiyo ipatayo 150, huku Unguja kukiwa na misumeno zaidi ya 120.
 
Amefahamisha kuwa takriban ekari 1000 za miti hupotea kila mwaka visiwani Zanzibar kutokana na kukatwa ovyo na kuongezeka kwa kasi hiyo kutokana na matumizi ya misumeno ya moto.
 
Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili Mtumwa Kheir Mbarak, amesema misumeno hiyo ambayo ni adui wa muda mrefu wa mazingira, inaweza kuiweza kuifanya nchi kuwa jangwa kwa muda mfupi na ni hatari pia kwa afya ya binadamu.
 
Maalim Seif yuko kisiwani Pemba kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambako anatembelea shughuli za kilimo kwa lengo la kuwahamasisha wakulima kuendeleza kilimo chenye tija kwa kutumia utaalamu wa kisasa na mbegu bora.
 
Katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambako alianza ziara yake alitembelea shamba la utafiti wa uzalishaji wa mpunga wa mbegu ya nerika liloko Gombeume mchangamdogo, skuli ya wakulima iliyoko Kiongweni Kambini, shamba la viazi vitamu Makangale na skuli ya wakulima juu ya nishati mbadala iliyoko Kinyasini.

4 comments:

  1. Busara itumike zaidi kutunga sheria hii kuliko munkar. Msumeno, kama zana, hauna tofauti yeyote na shoka, panga au mundu. Msumeno pia ni nyenzo nzuri ya kuleta maendeleo kwa njia ya haraka. Misumeno pia inatumika kwenye uokoaji kwa kukata haraka magogo na vyuma vidogovidogo ili waokoaji wapite kwa haraka.Kinachohitaji ni kuweka na kuilinda sheria ya matumizi yake na sio kuichoma moto. Hapa panaonyesha pana udhaifu wa kuzisimamia sheria zetu na ndio maana tunafikia hapa.

    Ingetumika fikra kidogo tu, basi angalau hiyo misumeno tungeiuza nchi za nje tukapata pesa za kigeni au hata kuibomoa na kufanya recycling. Hapo tumechoma utajiri kwa ukosefu wa kutumia busara kama itakiwavyo.

    ReplyDelete
  2. Hongera Maalim kwa kazi nzuri, tunakumbuka kabla huja fukuzwa uwazirikiongozi,ulikwenda kwunu pemba mkoani ukachoma ngara za wanyenge ilikuwa kama kafara nawewe ukafukuzwa uwaziri kiongozi.Pengine ving"ora vshakutosha unafanya vituvyako

    ReplyDelete
  3. A/a !!! Sad people always utawajuwa chuki katika roho!! Mkimchukia mtu ayeumia sio unayemchukia but yourself ...!!!!! So just be happy na ondoa chuki katika roho you will be a happy person!!!

    ReplyDelete
  4. Jamni huu ni ukweli si uhasidi wala choyo, alizi choma keli ngara za masikini kwa kisngizio cha magendo, mmesahuutu kwa kuwa yeye sasa mkubwa ana ving'ora

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.