Na Husna Sheha.
TIMU ya Mtoni United ya Mtoni imekabidhiwa kitita cha shilingi laki tano na kikombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye ligi daraja la pili Wilaya Magharibi.
Aidha, timu ya Muungano imetia kibindoni shilingi laki tau kwa kushika nafasi ya pili michuano hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Wilaya ya Magharibi Ali Suleiman Mohammed, ndiye aliyekabidhi zawadi hizo katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa meli saba Bububu, sambamba na mpira mmoja kwa kila timu.
Akitoa nasaha zake, Mwenyekiti huyo alizitaka timu za wilaya hiyo kujitahidi katika mashindano ya taifa ili kuiweka katika ramani nzuri wilaya hiyo.
Alieleza kuwa, ZFA wilayani humo imeamua kujipanga upya ili kuziinua timu zake na kuiwakilisha vyema wilaya yao.Michuano hiyo ilishirikisha timu 37 zilizokuwa zimepangwa katika makundi matatu
No comments:
Post a Comment