Habari za Punde

Simba yatimuliwa Chukwani . Kihwelu asema wana uhakika wa magoli matatu

Na Mwandishi Wetu
KLABU ya Simba SC, imelazimika kuhamishia mazoezi yake katika uwanja wa Mao Dzetung baada ya uongozi wa Chuo cha Elimu Chukwani kudai hauna taarifa ya kutakiwa uwanja huo na wekundu hao.

Aidha, uongozi wa chuo hicho umesema umeamua kuufunga uwanja wake huo kwa ajili ya kuufanyia matengenezo.

Hata hivyo jana asubuhi, wekundu hao walifanya mazoezi katika uwanja huo, na baadae jioni kuhamia Mao Dzetung baada ya uongozi wa chuo kutoa taarifa ya kuufunga uwanja wake.

Mmoja wa watendaji wa chuo hicho ambaye hakutaka kutajwa kwa kuwa si msemaji wake, alithibitisha kuzuiliwa kwa Simba kufanya mazoezi uwanjani hapo baada ya kuutumia asubuhi jana, akidai kuwa walivamia bila ya taarifa.

“Hawa wamejenga mazoea kila wanapokuja Zanzibar kutumia uwanja wetu, sisi hatuna taarifa, leo (jana) asubuhi tumewakuta tayari wako uwanjani, lakini tumefanya uungwana na kuwaachia wamalize, na baada ya hapo tunaufunga kwa ajili ya matengenezo”, kilisema chanzo chetu.

Alipoulizwa, mratibu wa ziara ya Simba hapa Zanzibar Abdul Mshangama, alikanusha kutimuliwa kwa kikosi hicho katika uwanja wao, na kusema kuwa kauli hiyo inalenga kuichafua kisaikolojia timu yake.

Hata hivyo, alikiri kuwa nusu ya uwanja huo kwa sasa imechimbuliwa, na Simba jana walifanya mazoezi katika sehemu iliyobaki.

Alisema, kama uongozi wa chuo hicho ungekuwa umewafukuza, wasingewea kufanya mazoezi jana, lakini wameona kutokana na hali ya uwanja ilivyo, ni bora waachane nao na kwenda Mao Dzetung.

“Simba imekuja Zanzibar kufanya mazoezi kwa utulivu na usalama zaidi, huenda hizo ni kauli za watu wasiotutakia mema ambao wanajaribu kutuvuruga kisaikilojia. Lakini hiyo si dawa na kambi yetu hii itasaidia kuharibu sherehe za ubingwa Yanga”, alijigamba Mshangama ambaye ni mwanachama kindakindaki wa wekundu wa Msimbazi. Wakati huohuo, akizungjmza nna gazeti hili jana kwenye uwnaja wa Mao Daetuhng, Kocha Msaidzii wa Simba Jamhuri Kihwelu, alijgama kuwa, ana hakkka wa kuifyunga Yanga magoli matau safi.

“Kwa kiwango cha vijana wetu, Yanga haiponi, kwanza haina wachezaji zaidi ya Frank Domayo na Athumani Iddi Chuji”, alijigamba Kihwelu maarufu kama Julio, mwenye kawaida ya kusema maneno mengi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.