Habari za Punde

Uwanja wa Mnazi Mmoja ulivyo kwa Sasa.

 Uwanja wa Michezo mkubwa kuliko yote katika visiwa vya Zenj ni huu uwanja wa mnazi mmoja ambao ulikuwa ukitowa nafasi kwa timu zote za Zanzibar zilikuwa zikifanya mazoezi katika uwanja huu.
Enzi hizo ulivyokuwa na hadhi yake na kiwango cha mpira katika Zanzibar ulikuwa uko juu. Na kutamba katika michuano za Gossage na michuano mengine nje ya Zanzibar na Ndani.
Na kuwa na upinzani wa timu za ndani wakati huo kulikuwa na Timu za Miembeni, Malindi, Vikokotoni, Ujamaa Mwembeladu, Kikwajuni ,Usawa,  Jeshi,  KmKm na nyenginezo zilizochipukia kama Small Simba, Nyuki, Black Fighters, Everton, na nyengine zilikuwa na ushindani wa hali ya juu na kuwa na kiwango kikubwa katika mchezo wa mpira. Na takriban zote zilikuwa zikifanya mazoezi katika viwanja hivyi.
Taasisi husika inabidi kukifanyia matengenezo ili kuweza kukirudisha katika hali yake ya zamani na kutumika kama viwanja vyengine katika Zanzibar.
Viwanja vingi vimekufa na kufanya maeneo ya kulazia magari na kuwa na matumizi madogo kwa shughuli za michezo kama vile kiwanja cha kibanda maiti kilikuwa kikitowa huduma ya michezo kwa timu za African Kids na timu nyengine.

ZFA inatakiwa kufanya jitihada za makusudi kuvirejesha viwanja hivi katika hali yake ya zamani na kuweza kurudisha kiwango cha michezo kama zamani na kuipa Zanzibar hadhi yake ya mchezo wa mpira wa miguu.

3 comments:

  1. Nashukuru muandi kwa kuliona hili la uwanja wa mnazimmoja, lakini sisi Wazanzibar ni watu wa ajabu sana tuna mbombo mingi ya kujishulisha nayo,likini hatuhoji kaziyetu kuluumu Zfa, wakati viwanja hatuna wala hatuna bidiiya kuwanoa vijana kwa michezo .Tutakumbuka vitu adim kama viwanja,















    t












    ReplyDelete
  2. Brother Othman ,Umenifanya machozi yanilengelenge kwani katika udogo wangu nikiwa nafatilia mambo ya michezo Alikuwepo Jaamaa mmoja marufu sana hapa Zanzibar Akitwa Abedi Suba alikuwa ni mwendaji mbio sana katika mashindano ya maskuli ya mbio kama kumbukumbu zangu zipo sawa kuna siku alikuwa katika mashindano hayo ya mbio tukawa tunamshangilia Suba suba akiwa usoni wa kwanza basi kwa uchepe wa wazanzibari kwa wakati ule alikatisha zile mbio nakueleke pwani huku watu wakishanga ilikuwaje alipo ulizwa akasema tumbo la kuharisha lilimshika ,huo ulikuwa ni wakati wa raha zanzibar sijuwi kaishia wapi naimani yuhai Mungu ambariki alikuwa ni kiioo kwetu sisi wadogo zake

    ReplyDelete
  3. Kwa ufupi Zanzibar mambo hayaendi!!!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.