Na Mwantanga Ame
SIKU moja baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusoma bajeti yake, baadhi ya wananchi wamekataa wazo la serikali la kuongeza posho kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na badala yake inapaswa kuiimarisha sekta ya afya ikiwemo kuongeza madaktari, elimu na kupunguza kodi kwa wafanyakazi wa umma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), Khamis Mwinyi akizungumza na Zanzibar Leo, alisema ingawa serikali inaweza kutekeleza mpango huo lakini bado inahitaji kujipa muda ili iweze kuziimarisha sekta nyengine.
Alisema baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Kenya, imeanza kuingia kwenye machafuko baada ya serikali kuwaza kutekeleza mpango huo ambao unapingwa na wananchi.
Alisema wakati wa maandalizi ya bajeti hiyo, ZATUC iliishauri serikali kusubiri kutekeleza wazo hilo, lakini ushauri wao umepuuzwa.
Alisema ingawa bajeti imeweza kuonesha maeneo ya kufanyiwa kazi moja kwa moja katika baadhi ya sekta za huduma ya jamii zikiwemo za maji, ujenzi wa barabara na huduma za afya, lakini bado kunahitajika ubunifu wa kuongeza ajira.
Aidha, alisema serikali inapaswa kuliangalia suala la kodi zinazotozwa wafanyakazi wa umma kwa vile inaonekana wanalipa kiasi kikubwa cha fedha ikilinganishwa na wananchi wa kawaida.
Akifafanua kauli hiyo alisema mfanyakazi wa serikali hivi sasa analipa kodi kutoka katika mshahara wake lakini hapo hapo amekuwa akilipia kodi katika ununuzi wa bidhaa.
Kutokana na hali hiyo, Katibu huyo alisema ni vyema serikali ikaliangalia suala hilo ili kuona namna ya kuwasaidia wafanyakazi wa kawaida kwani bado vipato vyao viko chini.
Nae Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, aliipongeza serikali kwa kuzingatia mishahara ya watumishi wa umma kwa sababu kipato chao kiko chini mno.
Alisema ingawa serikali imewaza hilo, lakini bajeti mpya bado itashindwa kustawisha maendeleo ya jamii na badala yake kufikiria kuongeza posho kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Alisema haieleweki hivi sasa kuna uhalisia gani juu ya kutekeleza azma hiyo kwa kuziangalia kada nyengine kama taasisi maalum, ikiwemo ya madaktari na walimu.
Alisema serikali inahitaji kujipa muda wa kutekeleza mpango huo kwa kuangalia vipaumbele vya kada nyengine kama vile ya wafanyakazi ngazi ya chini, madaktari na walimu na sio ngazi ya viongozi kwa vile mwaka uliopita kulikuwa na mapendekezo yaliotolewa kwa ngazi hizo.
Alisema bajeti mpya inaonekana kukosa mwelekeo wa kutoa ubunifu wa mipango mipya ya maendeleo itakayoonesha ni sekta gani zitaongeza ajira na kukuza pato la taifa zaidi ya kuwapandishia kodi wananchi.
Kuhusu baadhi ya kodi zilizopandishwa ikiwemo ya magari, Mwakilishi huyo alisema nalo bado linahitaji kuangaliwa kwa upande mwengine kwa kubuni vyanzo vipya vya kodi kwa kuwa hivi sasa wahusika wanalipa kodi zipatazo 15.
Aliishauri serikali kusimamia mgao wake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kodi mpya kwa wafanyakazi wa Muungano kwani kuna taarifa fedha hizo hazijaingizwa katika mfuko mkuu wa serikali.
Nae Katibu wa Chama cha TADEA Zanzibar, Juma Ali Khatib, akizungumzia bajeti hiyo alisema ingawa imeonesha mwanga mzuri wa kupunguza tatizo la ajira, lakini serikali inapaswa kuangalia namna ya kutekeleza wazo la kuongeza posho kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwani bado sio wakati muafaka.
Alisema hivi sasa sekta ya elimu inaonekana haina ustawi wa moja kwa moja pamoja na sekta ya afya kwa kukosa kuwa na vifaa vya msingi vikiwemo madeski na vifaa vya kufundishia zikiwemo maabara huku maslahi ya walimu na madaktari yakiwa bado madogo.
Aidha, alisema hatua ya serikali kushusha kiwango cha ushuru kwa bidhaa za unga na mchele, ni jambo la kupongezwa lakini alisema ushuru huo ulikuwa ufutwe kabisa.
Nae kada wa CCM, Fatma Khamis, alisema bajeti mpya imeonesha mwelekeo wa kuimarisha uchumi na kudhibiti ukwepaji kodi, jambo ambalo litaiwezesha serikali kufanikisha malengo yake.
Navipongeza Vyama vya Ushirika wa Wafanya kazi Zanzibar kwa juhgudi zao zakukataa Kuongezwa kwa Maposho MBLW. Hatujaona Kazi waliowafanyia Wananmchi . Kwanini waongezwe Maposho yasiokua na Maana wakati kuna Watu hawamiliki hata mlo mmoja?
ReplyDeleteUjinga wa Serikali huo kuwanenepesha Wawakilishi na Mawaziri ili wapate Kuilinda CCM- Tunataka Huduma za Maendeleo kwanza na kuleta Miuondo mbinu sio kuongezwa Maposho kwa Viongozi na Member wa Baraza la Mapinduzi wakazidi kunyanyasa Watu.
Kwanza wenge tueleza bajetihi pesa zimepatikana wapi msada au kodi za wananchi,halafu watwambie, mchango wa jamhuri ya muungano kwa bajeti ya zanzibar.Tunamushikeli, tanusifu bajeti hilkuwa tunajua mambo hayaendi vizuri.Mwaka ulopita bajeti kama hii hakuna kilofanyika, matumizi mabovu naufujaji ndini ya ofisi za smz, hakuna wakuukemea,leo, mh,anase,kipaumbe, afya na elimu, hasemi ,smz, inakushanya watu, walokwisha staf, kuitumikia,nchi hawa wezitena, utasikia kateuliwa mkuu wa bodi wana fuja pesa za walipakodi buru,na nyie Cuf,muamsho hasemi au mlikuwa njaa zina kusumbueni sasa kimmya
ReplyDelete