Habari za Punde

Kamati ya Kuifufua Timu ya Kikwajuni Sauti ya Tembo Zenj..............

 Viongozi wa Kamati ya Kuifufua Timu ya Kikwajuni KSC.ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mzee Ali Hassan mwenye kazu nyeupe,  ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza Mkutano wao wa mkakati wa maandalizi ya kuhakikisha timu hiyo inarejea katika Ligi Kuu ya Zanzibar, wakiwa nje ya Klabu hiyo ilioko katika mtaa wa Kikwajuni Zanzibar. 
 Viongozi wa Kamati ya kuhakikisha timu yao ya KSC inarejea katika Ligi Kuu ya Zanzibar na kusikika kama zamani wakiwa nje ya Klabu hiyo wakiwa katika mikakati yao na kubadilishana mawazo. 



Viongozi wa Kamati ya Kuirejesha Kikwajuni katika Madani ya Soka la Zanzibar wakiwa katika moja ya kibaraza katika klabu hiyo wakibadilishana mawazo jinsi ya kuirejesha timu  hiyo katika medali ya soka la Zanzibar, kwa kipindi kirefu kuzolota kwa timu hiyo.kutoka kushoto Dingo, Ndevu , Suleiman Mahmoud Jabir, Kocha Hafidh Badru na Kocha Burhan Msoma Mkubwa.

5 comments:

  1. Hiyo picha haifanani na Nembo ya Kikwajuni. Kwanini waweke Nembo ya Tembo na ilhali Zanzibar hakuna Tembo?

    Mimi nachukiwa sana na watu wanaopenda kujipaka paka na vitu wasivomiliki.

    Kwanini wasichjore picha ya Jogoo hapo na Mpira? Inaweza kuleta sura nzuri kama vile Klub moja ya France.

    ReplyDelete
  2. Jamo la msingi kujiuliza kwa nini kikwajuni ilikufa! Sasa ni vyema mkajiepusha na hayo mambo yaliyoua kikwajuni. Mara nyingi kwenye jumuiya hizi za mipira na n.k wizi wa fedha ndio chanzo cha kuua hizi taasisi.

    ReplyDelete
  3. na isitoshe si kikwajuni tu timu nyingi zimekufa kwa mambo yao ya siasa.Siasa ilizoretesha soka ya zanzibar hasa zile timu zilizokuwa zinadaiwa kama viongozi wao ni sapoter wa vyama vya upinzani,zanzibarar fitna,majungu,lakini pia na vitisho,ikiwa pamoja na kuzuiliwa biashara zao wale wafadhili waliokuwa wakizifadhili timu hizo, lakini sasa kwa uwezo wa mungu yote hayo yanaelekea ukingoni.sasa ningependa kuwasihi viongozi wote wale wa timu za zanzibar,kikwajuni small simba malindi shangani na nyingine warudi wakaziimarishe tena timu zao iwe kama zamani wakati ndio huu hadhi yazanzibar itajirudia kesho mungu ibariki zanzibar

    ReplyDelete
  4. Penye na pana Njia wana wa kikwajuni tujumuike pamoja kuinua timu ya tu ya Mtaa....Mtu huringia chake !

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.