Habari za Punde

Siku ya mazingira ilivyoadhimishwa Pemba

 WAFANYAKAZI wa Idara ya Mazingira Pemba, wakichoma moto mataka waliyoyakusanya katika mji wa Chake Chake, katika kilele cha siku ya Mazingira Duniani, maara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi katika mji huo
 BORDOZA la Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba, likihamisha Jaa maarufu la kutupia taka, huko vitongoji katika siku ya Mazingira Duniani, na kutafutwa sehemu nyengine ya kutupia taka.
 WAFANYAKAZI wa Baraza la Mji Wete, wakikusana na kuhamisha taka, zilizotupwa katika jaa lililokuwa sio rasmi, ambalo limeibuliwa na wananchi, huko katika kijiji cha Migombani wete
 MWANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Jadida Wete, Yussuf Ali wa darasa la Saba “B”, akipanda Mti katika eneo ambalo linaharibiwa na Maji ya Mvua, katika siku ya Mazingira Duniani
 Afisa Elimu Wilaya ya Wete Khamis Said Hamad, akimkabidhi Cheti cha uandihsi bora wa Insha juu ya  umuhimu wa kutunza Mazingira, mwanafunzi wa Skuli ya Msingi Makangale Asha Darus Faki, katika siku ya Mazindira Duniani
WAFANYAKAZI wa Idara ya Mazingira Pemba, wakiangalia Jaa linalotupwa taka, ambalo limemegwa na Maji ya Bahari huku likiwa karibu na makaazi ya watu, kama linavyoonekana katika Picha. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

1 comment:

  1. Hongera sana muandishi kwa kutuwekea habari hii.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.