MADAKTARI wa kihispania, wanaofanya kazi
katika Hospitali ya Chake Chake Pemba, wakimtibu mmoja ya majeruhi wa ajali ya
Gari iliyotokea Pondeani, Massoud Ali Said (10), ambaye ameumia mkono wa
kushoto, na kusafirishwa kupelekwa katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani kwa
matibabu zaidi. (Picha na Abdi Suleiman,
Pemba)
Na Abdi Suleiman, Pemba.
JUMLA ya watu nane (8), wamenusurika kupoteza maisha, akiwemo mtoto mdogo mwenye umri wa miaka Miwili na Nusu (2½), baada ya gari ya abiria aina ya Toyota, yenye namba za usajili, Z196 BB, kupinduka, katika maeneo ya Pondeani, Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba.
Ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi (jana) majira ya saa nne na dakika Arubaini na Saba (4:47), gari hiyo iliyokuwa ikitokea Wesha kwenda Mjini Chake, huko Pondeani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Saleh Mohammed Saleh, amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na Uzembe wa dereva wa gari hiyo, aliyekuwa akifukuzana na gari nyengine.
Kamanda Saleh alisema kuwa, baada ya kutokea kwa ajali hiyo dereva na utingo wake, wote walikimbia, huku jeshi la Polisi Mkoa wake likiendelea kuwatafuta na watakapopatikana watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Aidha alisema kuwa, katika ajali hiyo, hakuna mtu hata mmoja aliyepoteza maisha wala, kupoteza fahamu, huku hali za mejeruhi wote zikiwa ziko nzuri, na wakitarajia baadhi yao kupata ruhusa.
“baada ya kutokea ajali dereva na konda wake wote wamekimbia, ila jeshi la polisi linawatafuta na pindi wakipatikana, tutawachukulia hatua za kisheria, ila sasa akari wako katika upelelezi na kupima sehemu ya ajali ilipotokea”alisema kamanda Saleh.
Aidha aliwataja majeruhi hao, kuwa ni Asha Juma Hamad (45), Mariyam Omar Ali (20), Khalid Said Ali (5), Zuhura Khalfani Salum (70), Massoud Ali Said (10), Akhalam Mbarouk Issa (2½), Saumu Hassan Salum (40) na Zuwena Faki Haji (24), wote ni wakaazi wa Wesha wilaya ya Chake Chake.
Hata hivyo, kamanda aliwataka Maedereva wa gari za abiria kutii sheri bila ya shuruti, wakati wote wanapokuwa wamepakia abiria ndani ya gari zao.
Kwa upande wake Dk Suleiman Ali aliyewapokea majeruhi hao, alisema kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyefariki dunia na wala kupoteza fahamu, bali wote walipofika hospitali wakiwa na fahamu zao.
Alisema kuwa, tatizo kubwa lililowakumba majeruhi hao, ni mshutuko tu, kwani kila mmoja alikuwa na mshutuko wa hali yake, huku akiwa na wasiwasi na mmoja kati ya majehuru hao, Asha Juma kuwa bega leke limevunjika.
Alise alisema kuwa, na Mkono wa Massoud Ali Said (10), kuwa mkono wake umekatika ila uthibitisho zai wanao madaktari wa kihispania ambapo ndio watakaowatibu na kujuwa hali gani aliyonayo mgonjwa.
Zanzibar leo ilipiga hodi katika woti ya watoto, aliyolazwa Massoud Ali Said, na kufanikiwa kuwakuta madaktari wa kihispania wakiwa katika harakati za kumpa huduma ya mwanzo mgonjwa huyo.
Aidha baada ya kumalizika madaktari hao, waliamua kumsafirisha na kumpeleka katika Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani kwa matibabu zaidi, gari hiyo ya abiria iliyokuwa ikitokea wesha kuelekea mjini ilikuwa ikiendeshwa na dereva, Zahor Khamis Mohammed na utingo wake Ali Khamis Mohammed.
No comments:
Post a Comment